Header Ads

Mkurugenzi, Watumishi watakiwa kushirikiana



Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro wametakiwa kushirikiana katika kuinua taaluma sambamba na kuboresha miundombinu ya Elimu katika Halmashauri yao.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro Mhandisi Joyce Baravuga wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ambapo alitembelea shule za Sekondari Njungwa na Nongwe ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika Halmashauri zote za Mkoani humo.
Ziara hiyo iliyokuwa na lengo la kukagua maendeleo ya shule za Sekondari kupitia vigezo 21 vya kutathimini utendaji kazi shuleni ili kwenda sambamba na Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro kutaka kufahamu sakata la kuuzwa bati zilizonunuliwa kwa fedha ya Serikali kwa ajili ya ujenzi  wa madarasa na nyumba za walimu katika Shule hizo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo Agnes Mkandya alikiri kuwepo kwa sakata ambalo lilimfanya kumvua madaraka ya Ukuu wa shule na kuwa mwalimu wa kawaida kwasababu ya kukiuka taratibu za Serikali na matumizi mabaya ya mali za Serikali licha ya kuwa hilo lilifanyika kwa lengo la kulipa madeni yaliyotokana na ujenzi wa shule hiyo.
“nikweli tatizo hilo limetokea ambapo kulikuwepo bati ambazo zilibaki baada ya kukamilika ujenzi wa madarasa matatu na nyumba za walimu katika shule hizi, lakini wakuu wa shule waliuza bati hizo wakidaikulikuwepomadeni ya mafundi waliojenga majengo hayo pasipo kufahamu mali ya  Serikali  huwa haiuzwi”, Alisema Mkandya.
Mhandisi Baravuga pamoja na lengo la kukagua maendeleo ya shule hizo kitaaluma kupitia vigezo 21  alilazimika pia kutatua mgogoro uliopo kati Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo na Wakuu wa Shule za Sekondari za Nongwe na Njungwa ambao walisimamia Ujenzi uliokuwa unaendelea katika shule zao na kuvuliwa madaraka yao.
Mhandisi Baravuga aliwataka walimu hao sambamba na Mkurugenzi wao ambaye ndiye kiutendaji ni bosi wao kushirikiana na kuhakikisha wanainua kiwango cha taaluma katika shule hiyo na Wilaya yao kwa jumla.
Ziara hiyo ya Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro ni mwendelezo wa ziara zake katika Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro zenye lengo la kukagua maendeleo ya shule na kufikisha vigezo 21 vya kutathmini maendeleo na utendaji kazi shuleni ambapo tayari ameshatembelea Halmashuri za Wilaya za Kilombero na Kilosa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.