Header Ads

RC MOROGORO AZITAKA HALMASHAURI ZOTE KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA WAKATI WA UTOAJI VIBALI VYA UJENZI.

RC Sanare akizungumza katika kikao cha 36 cha Bodi ya Barabara leo.


MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare, amezitaka Halmshauri zote za Mkoa wa Morogoro kufuata taratibu za kisheria wakati wa kutoa Vibali vya Ujenzi.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Desemba 19, 2019,  katika kikao cha 36 cha Bodi ya Barabara,  amesema lengo la kufuata sheria itasaidia kuepusha wimbi kubwa la Wananchi wanaojenga nyumba zao barabarani.

"TANROADS wamekuwa wakibomoa majengo yanayokuwa yamejengwa kwenye hifadhi ya barabara, huku vibali vya ujenzi vikitolewa na Watumishi wa Halmshauri husika jambo ambalo nataka lisiendelee kutokea katika Mkoa wangu" Amesema RC Sanare.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.