MKURUGENZI Manispaa Morogoro awataka Watumishi wa Kike kulitumia Sanduku la Maoni kukomesha unyanyasaji wa Kijinsia kazini..
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema kuwepo kwa Sanduku la maoni kutawafanya Watumishi Serikalini na Sekta binafsi kuwa huru kutoa Maoni dhidi ya vitendo viovu.
Hayo ameyasema leo Desemba 3, 2019, wakati Jamii ikiwa ndani ya maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Jinsia Duniani.
Aidha amesema kuwa, dhumuni la Sanduku hilo ni kuwafanya Watumishi kutoa Taarifa ya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia .
Katika upande mwengine, amesema matendo ya ukatili wa jinsia yanafanywa sana na wanaume hivyo uwepo kwa Sanduku la maoni litawafanya Watumishi wakike kuwa huru huku akisema kwamba wale wote watakaobainika kuwa na tabia hiyo watachukuliwa hatua Kali za kisheria .
Amesema kitendo cha unyanyasaji Wa kijinsia ni kinyume na Sharia ya ajira na mahusiano kazi Namba 6 ya mwaka 2004.
" Najua Sanduku hili lipo hapa lakini katika siku hizi za Kupinga Ukatili wa Jinsia tuanze kutambua umuhimu wa Sanduku hilo , tumelifunga hapa Ofisini kwa kuzingatia eneo litakalofikika kwa watu wote na ndugu zetu wenye ulemavu wapate fursa ya kutoa maoni yao, tunamshukuru Mkuu wetu wa Wilaya, Mhe. Regina Chonjo kwa kuwa karibu na Wanawake hii inaonesha ni kwa jinsi gani anatekeleza vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuelekea Uchumi Wa kati na Tanzania ya Viwanda kwa kuwawezesha Wanawake , Wakina mama, Vijana na Walemavu" Amesema Sheila.
Amesema kuwa miongoni mwa Vitendo wanavyokutana navyo Watumishi Wa kike ni pamoja na Rushwa ya ngono , udharirishaji Wa kijinsia na kudharaurika.
Ikumbukwe kwamba agizo hilo lilitolewa kwa Halmashauri pamoja na Manispaa zote kwa makatibu Wa Wilaya kufanikisha kuwepo kwa Sanduku la Maoni ambapo Manispaa ya Morogoro ilianza mapema kumkomboa Mwanamke.
Post a Comment