Header Ads

MOREPEO YAKABIDHI VIFAA TIBA KWA WAZEE VYENYE THAMANI YA TSH MILIONI 14


Afisa Utumishi Manispaa ya Morogoro, Ndg. Waziri Kombo (watatu kutika kulia) akipokea Vifaa Tiba kwa ajili ya huduma kwa Wazee kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa kutoka Shirika la MOREPEO leo Desemba 6,2019 nje ya Ofisi ya Manispaa ya Morogoro, (kulia) Katibu wa Muungano wa mashirika ya kuwahudumia wazee Tanzania "Tanzania Older Peaples Platform"(TOP), Wilson Karuwesa. 

HALMSHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepokea Vifaa Tiba vya kuhudumia Wazee vyenye thamani  ya Tsh Milioni 14 kutoka Shirika lisilo la Kiserikali NGO la MOREPEO kwa ajili ya kutolea huduma kwa Wazee katika Jamii.
Akizungumza na Waandishi wa habari katika hafla fupi ya upokeaji wa Vifaa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa, Waziri Kombo, ametoa shukrani, huku akisema licha ya msaada huo shirika hilo la MOREPEO limekuwa msaada mkubwa katika kuwahudumia Wazee wa Manispaa ya Morogoro.
Amesema miongoni mwa huduma za Shirika hilo wanazozitoa katika Manispaa ya Morogoro ni kuwahudumia Wazee ,  lakini zaidi wamekuwa wakisaidia Manispaa katika shughuli mbali mbali kwa kutumia fedha zao wenyewe.
Aidha , amesema licha ya kutoa vifaa hivyo lakini wamewarahisishia kuwapa mafunzo watoaji wa huduma za afya  ngazi ya jamii , hivyo watahakikisha wanawasisitizia vifaa hivyo viweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
"Mimi nalifahamu sana Shirika hili  tangia miaka 10 au zaidi iliyopita, wamekuwa wakitusaidia sana hususani katika utoaji wa Vitambulisho vya Wazee wamekuwa kipaumbele sana , lakini niseme hata sisi tutakuwa wazee kwa kuwa tunakaribia, niwahakikishie Wazee wangu  kwamba sisi kwa  upande wa Manispaa tunatambua umuhimu wa Wazee hivyo kuwasaidia kuwahudumia wazee wenzenu ni jambo jema na ni jambo la mfano nasi tunashukuru, Mganga Mkuu tumepewa vifaa hivi tuvitumie vizuri ili nasi tuoneshe shukrani yetu kwa kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa  "" Amesema Waziri Kombo
Amelitaka Shirika hilo liendelee na moyo wa kuwasaidia , kwani Halmashauri ina mambo mengi sana haiwezi kutekeleza kila kitu ingawa majukumu yao yanawapasa kufanya hivyo, kwahiyo  kama wadau wanazidi kujitokeza basi hakika manispaa  itaendelea kupiga hatua katika maendeleo.
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dk. Ikaji Rashid, amesema  kuwa kama inavyofahamika kwamba Wazee kadri umri unavyozidi kwenda mbele magonjwa  yanazidi kuwa mengi , kwahiyo vifaa hivyo vitawafikia na kuwapa huduma Wazee kwenye maeneo yale yale wanayoishi mitaani.
Aidha amesema katika vifaa alivyopokea miongoni mwa vifaa hivyo ni pamoja na Mashine ya kupima shinikizo la damu (Blood pressure), mashine ya kupima wingi wa Sukari kwenye damu, Olive Oil mafuta ya kufanyia masaji ambayo ni mazuri kwa afya ya moyo ,  Mashine ya kupima uzito ambayo itasaidia kuona nani ambaye lishe yake ni kubwa zaidi na dawa ya kusafishia vidonda inayoitwa hydrogen Peroxide ambayo itawawezesha wazee wenye matatizo madogo madogo kufanyiwa usafi pasipo kwenda katika ngazi ya vituo vya huduma za afya,Pia amesema sambamba na vifaa hivyo ipo spiriti na pamba kwa ajili ya kutumika kumsafisha mgonjwa kabla hajampima ugonjwa.
""Tumepokea vifaa kutoka shirika la MOROPEO ambalo linajihusisha na huduma za afya kwa wazee katika Mkoa wa Morogoro , na vimegawiwa kwa Ngazi ya watoa huduma kwa jamii (HBC) , baada ya kufanyiwa mafunzo yatakayowawezesha kuwapa huduma wazee ambao wapo mitaani.
Naye Katibu wa Muungano wa mashirika ya kuwahudumia wazee Tanzania "Tanzania Older Peaples Platform"(TOP), Wilson Karuwesa. amesema wamefika Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kuwakabidhi vifaa vitakavyotumika kwa ajili ya kutoa huduma kwa wazee, vifaa hivi vimetoka katika shirikia la BMZ lililopo Ujerumani  lenye kushughulika na kuboresha afya za wazee katika bara la Afrika.
Amesema thamani ya vifaa vyote walivyovitoa katika mkoa wa Morogoro ni Shilingi Bilioni 1,12,000,000/= , hivyo amemuomba Mkurugenzi kuwagawia  HBC wote ili waweze kuwahudumia wazee majumbani kwao.
" Vifaa hivi tumevitoa katika wilaya nane 8 za Mkoa wa Morogoro isipokuwa Wilaya ya Uranga kwa lengo la kuwahudumia na kuwatibu wazee katika jamii zao ambapo kwa kila Wilaya tumegawa mifuko 40 vyenye vifaa tiba kwa kila mfuko ukiwa na thamani ya shilingi laki 350,000/=" Amesema Karuwesa.
Amesema kwa mkoa mzima wa Morogoro waliwapatia mafunzo wahudumu wa afya ngazi ya Jamii (HBC)  wapatao 320, huku kila wilaya waliwapatia mafunzo HBC  40 kwa kila halmsahuri za manispaa zilizopo mkoani Morogoro.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.