Header Ads

JUMLA YA SHILINGI MILIONI 774 KUTUMIKA KATIKA UJENZI WA MTO KIKUNDI MANISPAA YA MOROGORO


Mafundi wakiendelea na Ujenzi wa Mto Kikundi.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro kupitia fedha za mkopo wa Benki ya Dunia chini ya fedha za  uboreshaji Miji ( Urban Local Government Strengthening Program (ULGSP) , imetenga jumla ya Shilingi Milioni 774 kwa ajili ya ujenzi wa Mto Kikundi ambao ulikuwa unaleta madhara kwa Wananchi pindi mvua zinaponyesha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja wa TARURA, Mhandisi,James Mnene, amesema ujenzi huo umeshaanza na hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 33% ya utekelezaji.
Mhandisi Mnene amesema mradi huo  utachukua miezi 3 ya utekelezaji ambapo ulianza tarehe 24, Oktoba, 2019 na unatarajia kumalizika Januari 22, 2019.

“Nimeridhishwa na kasi ya mradi huu, kiukweli mafundi pamoja na Msimamizi wa mradi wanajitahidi sana licha ya kuwepo na changamoto kama vile uwepo wa maji yanayotiririka na kusababisha kazi kua ngumu pamoja na mvua kubwa zinazonyesha baadhi ya mawe yaliyopangwa pembezoni mwa kingo yanaporomoka lakini matumaini yangu mradi huu utakamilika kwa muda uliopangwa”Amesema Eng. Mnene.
Kwa upande wa Msimamizi wa mradi kwa niaba ya Meneja wa mradi, Eng. Mboka Macknon, amesema hali ya mradi unaendelea vizuri, hivyo matarajio yao ni kuona wanafanya kazi kwa kasi kubwa ili kumaliza kwa wakati uliopangwa.
Pia amesema ujenzi huo wa mradi wa Mto Kikundi wenye KM 1,  unajumuisha kujenga kingo za mto , pamoja na kumwaga zege ambalo litawekwa nondo chini ya Mto.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.