Header Ads

Picha mbali mbali zikionesha matukio ya ugawaji wa zawadi kwa Waalimu na Wanafunzi waliofanya vizuri kwa ufaulu Shule za Msingi Manispaa ya Morogoro leo Desemba 27, 2019.



Mkuu wa Wilaya , Mhe, Regina Chonjo akimkabidhi zawadi Mwanafunzi wa Shule ya Msingi aliyefaulu kwenda kidato cha kwanza mwaka 2019  kutoka Shule ya Msingi Kihonda Maghorofani Silvester Masele , mwanafunzi huyo amefanikiwa kujiunga na Shule ya Sekondari Elboro Arusha.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,  akimkabidhi zawadi mwalimu wa Shule ya Msingi Mazimbu 'A' baada ya Shule hiyo kufanya kwa upande wa shule za msingi matokeo ya kujiunga na kidato cha kwanza.
Mkuu wa Wilaya, Mhe. Regina Chonjo, akimkabidhi zawadi mwalimu wa Shule ya Msingi Mazimbu 'A' Zuhura Ahmad aliyefanya vizuri katika Somo la Sayansi kwa upande wa shule za msingi matokeo ya kujiunga na kidato cha kwanza.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Abdul Buheti akizungumza wakati wa kutaja takwimu za matokeo na viwango vya ufaulu Shule za Msingi Manispaa ya Morogoro kwa Wanafunzi waliojiunga na  kidato cha kwanza mwaka 2020.


Mstahiki Meya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga  (kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao Maalum  cha Baraza la Madiwani, kulia  Mhe. Abdulaziz Abood Mbunge wa Morogoro Mjini.

Diwani Kata ya Mwembesongo, Mhe. Kalungwana (katikati) akitetea jambo na diwani mwenzake huku kikao cha Baraza cha Kawaida Baraza la Madiwani kikiendelea.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akizungumza kabla ya zoezi la utoaji wa zawadi kwa waanafunzi waliofaulu vizuri kwenda kidato cha kwanza Manspaa ya Morogoro.

Mhe. Mbunge Viti maalum, Dr Christine Ishengoma.







Mkuu wa Wilaya, Mhe. Regina Chonjo, akimkabidhi zawadi mwalimu wa Shule ya Msingi Ndetembia baada ya Shule hiyo kufanya vizuri kwa upande wa shule za msingi matokeo ya kujiunga na kidato cha kwanza. 
Mkuu wa Wilaya, Mhe. Regina Chonjo, akimkabidhi zawadi mwalimu wa Shule ya Msingi Mwere 'A' baada ya Shule hiyo kufanya vizuri kwa upande wa shule za msingi matokeo ya kujiunga na kidato cha kwanza. 

Mkuu wa Wilaya, Mhe. Regina Chonjo, akimkabidhi zawadi mwalimu wa Shule ya Msingi Mazimbu 'A' Anitha Nathan aliyefanya vizuri katika Somo la Hisabati kwa upande wa shule za msingi matokeo ya kujiunga na kidato cha kwanza. 

Mhe. Abdulaziz Abood, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini akiwa na Mbunge Viti Maalumu , Dr Christine Gabriel Ishengoma wakifuatilia kwa umakini kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani na utoaji wa zawadi kwa Wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya Taifa Shule za Msingi Manispaa ya Morogoro mwaka 2019 na kujiunga Kidato cha kwanza.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.