Manispaa ya Morogoro yageuka chuo cha mafunzo miradi ya Kimkakati, Meya aeleza jinsi wanavyoweza kusimamia mapato.
HALMSHAURI ya Manispaa ya Morogoro, imezidi kuchanja mbuga katika utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati hii ni kufuatia wiki mbili hivi karibuni kutembelewa na Halmshauri mbili tofauti kwa wakati mmoja katika kujifunza namna ya ukusanyaji wa mapato na njia bora ya usimamizi wa miradi ya Kimaendeleo hususani miradi ya Kimkakati.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga,amesema kuwa Manispaa ya Morogoro ina miradi mikubwa mitatu ya kimkakati ukianzia Stendi ya Msamvu ambayo imeshaanza kufanya kazi, lakini pia Soko Kuu la kisasa ambalo linaendelea kujengwa na Stendi ya daladala.
Amesema kuwa katika Jengo la Stendi ya Msamvu ambacho ni kituo bora cha Mabasi Afrika Mashariki kilichojengwa na Kampuni ya Msamvu Property Ltd , waliingia ubia na LAPF kwahiyo fedha zinazopatikana zinaingia kwenye mfuko huo, na pia faida inayopatikana wanagawana na tangia stendi hiyo ianze kazi wameshagawana faida mara moja.
Aidha, amesema kuwa katika faida waliiyogawana walifanikiwa kutenga jumla ya Shilingi Milioni 140 , hivyo katika mgawanyo huo Manispaa waliweza kupata Shilingi Milioni 40 kwa kuwa waliwekeza asilimia 40% na LAPF walipata milioni 100 kwa uwekezaji wa asilimia 60 na zaidi.
Amesema kuwa miradi mengine ikikamilika wataweza kukusanya mapato makubwa ya vyanzo vya ndani kutoka shilingi Bilioni 6.7 za sasa hadi kufikia Bilioni 10 na zaidi.
""Mradi huu ni mkubwa lakini tuliingia ubia na LAPF kwa asilimia , wenzetu walivyowekeza zaidi wao wana asilimia 60 na sisi Manispaa tuna asilimia 40 lakini asilimia hii 40 ya kwetu ilipungua kutokana na wenzetu waliwekeza zaidi, kwahiyo katika kugawana wao walipata milioni 100 na sisi tukapata milioni 40, lakini bado fedha zipo benki kwa ajili ya kupata faida kubwa , kwahiyo miradi hii itatuongezea mapato makubwa sana katika Manispaa,mradi huu mhe. Rais alishasema urudi ndani ya manispaa inaweza kututoa kutoka kwenye bilioni 6.7 hadi kwenye bilioni 10 na kadhaa na hiyo inawezekana tunatarajia soko letu litaisha Mwezi 2 , Mwaka 2020 na soko hilo ni fedha za kimkakati hatudaiwi na mtu hivyo tutaanza kukusanya wenyewe na mapato ya Manispaa yataongezeka hata hivyo stendi ya daladala nayo itakamilika mwezi wa 5 mwaka 2020 na fedha hizo pia ni za kimkakati" Amesema Mhe. Kihanga
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Bariadi Mkoa wa Simiyu, Mhe. Robert Mgata, ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa usimamizi mzuri wa makusanyo ya kodi na njia bora ya kuendesha miradi.
Amesema lengo la kuja Morogoro, namna bora ya ukusanyaji wa mapato pamoja na usimamizi wa miradi , hivyo matumaini yake ni mara baada ya kurudi Bariadi wataenda kuweka njia bora ya usimamizi wa miaradi ili kuongeza ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri yao.
Aidha, amesema Halmshauri ya Mji Bariadi tayari imeaanza ujenzi wa Stendi Mpya ya Kisasa na mpaka sasa ujenzi huo upo asilimia 95 kukamilika.
Amesema kuwa walichokipata na elimu pana ya ukusanyaji wa kodi wanaamini kabisa watapiga hatua na pengine kuwa moja ya Stendi bora kabisa nchini Tanzania katika suala zima la ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa wa kutawala.
Post a Comment