Watendaji Manispaa Morogoro watakiwa kutatua kero na malalamiko ili kuleta mabadilko chanya kwa Jamii.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro, Bi. Erica Yegele, akiwa na Afisa Utumishi Manispaa ya Morogoro, Waziri Kombo. |
Watendaji wa Kata na Mitaa Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro, wametakiwa kushughulikia malalamiko na migogoro iliyoko katika maeneo yao ili iwe chachu ya maendeleo na kuleta mabadiliko chanya kwa Jamii.
Watumishi wa Manispaa ya Morogoro kutoka Ofisi ya Utumishi. |
Hayo yamezungumzwa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro, Bi. Erica Yegele kwenye kikao kazi cha kufunga mwaka kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa Morogoro leo Desemba 31,2019.
Amesema kuwa Watendaji wanatakiwa kuwasilisha mihutasari ya vikao vyao kwa wakati , ikiwamo kuzingatia muda, nyakati na kutoa ripoti zenye uhalisia.
Watendaji. |
Ametoa agizo kwa kila Mtendaji kuwa na daftari la rejesta za malalamiko na hatua walizochukua baada ya kupokea malalamiko ili kurahisisha utendaji kazi kwa kutoa huduma bora kwa Wananchi wao.
'Nawaomba watendaji mfanyekazi kwa bidii, hali si shwari katika maeneo yetu, pia suala la usalama bado hafifu mfano kata ya Mafiga , niwaombe wakusanyeni hao vibaka na kuwatafutia mradi wa pamoja nipo tayari kutoa hata pesa zangu za mfukoni ili usalama wa wananchi uimarike" Amesema Bi Yegela.
Katika hatua nyengine amelalamikia kushuka kwa nidhamu shuleni, hivyo amewataka Watendaji kujenga utaratibu wa kuzifikia shule na kuzungumza na Wanafunzi pamoja na Waalimu ili kujenga mazingira mazuri na rafiki kwa nidhamu za wanafunzi wa Manispaa ya Morogoro.
Aidha amesema ni wakati wa Watendaji kushiriki kikamilifu katika suala zima la usafi na kusimamia vyema vikundi vya kufanya usafi kwani hali ya usafi katika baadhi ya maeneo hairidhishi.
Pia amesema Manispaa ya Morogoro ipo chini kimapato, hivyo Watendaji washirikiane katika kusimamia vyema vyanzo vya mapato na kuifanya Halmshauri kujiendesha yenyewe bila ya kutegemea fedha kutoka kwa wafadhili na Serikali kuu.
Post a Comment