Header Ads

PICHA MBALI MBALI ZIKIONESHA KAMATI YA SIASA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYA YA MOROROGO WAKISHIRIKIANA NA KAMATI YA FEDHA MANISPAA YA MOROGORO KATIKA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO LEO 04, DESEMBA 2019.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro, Ndg. Fikiri Juma (wa nne  kutoka kulia) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kutembelea miradi Manispaa ya Morogoro, kulia mhandisi wa TARURA Manispaa Eng. James Mnene , wapili kulia , Afisa utumishi Manispaa Morogoro aliyekaimu nafasi ya Mkurugenzi , Ndg. Waziri Kombo leo Desemba 4, 2019. Picha Idara ya Habari. 

Shule ya Sekondari Morogoro ni Miongoni mwa Shule 17 Kongwe zilizobahatika kupewa fedha kwa ajili ya ukarabati kufuatia agizo  la Mhe. Rais Dkt. John Magufuli.

Choo cha Shule ya Sekondari Morogoro kwa upande wa A, Level , kilichofadhiliwa na Rotary International ni miongoni mwa miradi iliyotembelewa leo na Kamati ya Siasa CCM Wilaya Morogoro pamoja na Kmati ya Fedha Manispaa Morogoro.

Jengo la kulia Chakula cha Jioni Shule ya Sekondari Morogoro kwa upande wa A, Level .

Viongozi wakijadiliana na kusikiliza maelekezo kutoka kwa Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng. Juma Gwisu, katika Shule ya Sekondari Mji Mpya.



Mhandisi wa TARURA , Eng. James Mnene (aliyevaa shati la mistari) akitoa maelekezo kwa Viongozi na Wajumb wa Kmati ya Siasa CCM na Kmati ya fedha katika mradi wa Barabara ya Barakuda Mazimbu.

Viongozi wakikagua ujenzi unaoendelea wa kutengeneza  mifereji ya  barabara ya Barakuda Mazimbu. 

Viongozi wakiondoka katika Jengo la Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule Manispaa ya Morogoro, Jengo hilo limegharimu Jumla ya Shilingi Milioni 152 ikiwamo na ununuzi wa vifaa.


Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Ndg. Waziri Kombo aliyetangulia akiomgoza msafara katika kutembelea mradi wa Soko Kuu la Kisasa Morogoro.

Mafundi wakiendelea na kazi za kutengeneza Mfereji Mto Kikundi uligharimu Shilingi Milioni 774 na ujenzi huo unatarajia kumalizika tarehe 22, Januari 2020.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.