KAMATI ya Siasa CCM Wilaya Morogoro yaipongeza Manispaa ya Morogoro kwa kukamilisha kwa wakati mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule Manispaa ya Morogoro.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Morogoro, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM ,Fikiri Juma, (wa pili kutoka kulia) wakijadiliana jambo pamoja na Wajumbe wa Kamati ya fedha Manispaa ya Morogoro. |
Jengo la Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule Manispaa ya Morogoro lililotumia kiasi cha Shilingi Milioni 152. |
KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro, imeipongeza
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kufuatia kujenga kwa ubora na kasi kubwa
katika ujenzi wa mradi wa Ofisi ya
Uthibiti Ubora wa Shule Manispaa ya Morogoro.
Hayo yamezungumza na na Mwenyekiti wa CCM Wilaya
ya Morogoro, Ndg. Fikiri Juma , wakati wa ziara ya kutembelea miradi yote ya
maendeleo inayoendelea kutekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa Habari , amesema kasi
na ubora wa Ujenzi unaonesha dhahiri Manispaa imekimbizana na inastahili
pongezi ya hali ya juu kwani licha ya ubora lakini imeonesha ni jinsi gani
imezingatia thamani ya pesa iliyotumika.
Aidha, amesema kuwa kama viwango hivyo , vilivyotumika
katika mradi huo wa Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule vikitumika katika miradi
mingine Manispaa ya Morogoro itapiga hatua na kutoa huduma bora kwa Wananchi.
Amesema kuwa Ujenzi huo umeonesha thamani ya pesa
iliyotumika , hivyo ameiagiza Manispaa ya Morogoro kuhakikisha inasimamia
vizuri na miradi mingine inayoendelea kutekelezwa na ilie ambayo itatekelezwa.
Pia amemuomba Mthibiti wa Ubora wa Shule Manispaa
ya Morogoro kuhakikisha katika majukumu yao wanawashirikisha Manispaa , Maafisa
Elimu, Waalimu wakuu wa Shule, pamoja na Bodi za Shule ili kuangalia ni kwa
naamna gani wanaweza kufanya kazi pamoja na kuleta maendeleo chanya katika suala zima la taaluma Shuleni.
" Nafahamu kwamba mpo chini ya Wizara ya
elimu , shirikianeni na Manispaa , lakini niwaombe taaluma yoyote haiwezi
kupanda kama Mtoto hajapata chakula vizuri , licha ya kufanya uthibi ubora
lakini suala la lishe kwa wanafunzi ni jambo la kulipa kipaumbele sana, niwaombe
na kuwashauri katika vikao vyenu hakikisheni wajumbe wa bodi wanakwenda
kushirikiana na Madiwani ambao wana ushawishi mkubwa wa kuongea na Wazazi ili
waweze kuchangia chakula shuleni na watoto wafanye vizuri katika masomo
yao" Amesema Fikiri
Amesema kuwa Shule nyingi hapa nchini zimetumia
sana fedha katika ujenzi Mhe. Rais Dkt John Magufuli amejitahidi kuwekeza
katika mpango wa Elimu bure bila malipo, hivyo ni wajibu wa kuhakikisha pamoja
na ubora wa shule lakini matokeo yaonekane katika viwango vya ufaulu.
Hata hivyo, Mwenyekiti Fikiri amempongeza
Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng. Juma Gwisu kwa kazi nzuri anazozifanya
katika kusimamia ubora wa miradi.
Kwa upande wa Mthibiti wa Uthibi Ubora wa Shule
Manispaa ya Morogoro, Bi. Victoria Michael Bengesi, amesema kuwa Manispaa ya Morogoro ni miongoni mwa
Halmashuri 100 nchini, zilizo katika
mpango wa Serikali wa kujengewa Ofisi za Uthibi Ubora wa Shule Wilaya.
Amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa tarehe
1, Julai, 2019 kwa kipindi cha miezi mitatu ya utekelzaji hivyo kuchelewa kwake
kumechangiwa na baadhi ya chanagmoto kama vile kutokuwepo kwa maji eneo la
ujenzi, kuchelewa kwa vifaa kama vile Saruji na mabati kutoka kwa msambazaji
hasa wa Viwanda kwa takribani wiki mbili na kuchelewa kupatika kwa matofali
yanayofaa kutoka kwa msambazaji aliyeteuluiwa.
Amesema mradi huo umegharimu jumla ya Shilingi
Milioni 152 ambapo pesa hizo zimejumusiha gharama ya ujenzi pamoja na ununuzi
wa samani na vifaa.
"Utekelezaji wa mradi huu umekamilika kwa
asilimia 100, hivyo kwa sasa shughuli zinazoendelea ni pamoja na ufungaji wa
milango, upigaji wa rangi awamu ya mwisho, uwekaji wa marumaru eneo la vyoo vya
ndanipamoja na ufungaji wa mfumo wa umeme" Amesema Bi. Benge
Katika hatua nyengine, amesema licha ya shughuli hizo kuendelea , zipo
shughuli nyingine za zaiada ambazo zimeongezeka
kutokana na uhitaji na mazingira halisi ya ofisi ilipo.
Miongoni mwa shughuli hizo ni pamoja na Uwekaji
wa uzio kwa ajili ya usalama wa Ofisi, Ujenzi wa kibanda cha mlinzi, Ujenzi wa
Choo cha nje chenye matundiu mawili na Ujenzi wa Karavati ili kuwezesha
uingiaji na utokaji katika eneo la Ofisi kwa urahisi.
Post a Comment