Mkuu wa Wilaya, mkurugenzi Manispaa ya Morogoro wawakumbuka Watoto yatima na Wazee wasiojiweza kuelekea kukaribisha Mwaka mpya.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe.
Regina Chonjo, pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba wamefanya
matembezi ya kuwakumbuka Jamii kwa
kutekeleza utoaji wa zawadi za Vyakula na Vinywaji kwa Makao ya kulelea watoto
yatima cha MGOLOLE kilichopo wilaya ya Morogoro.
Akikabidhi vitu hivyo vyenye
thamani ya Shilingi Milioni 1,kwa upande wa Mkuu wa Wilaya, Mhe. Regina Chonjo,
amesema kuwa Ofisi yake ya Wilaya na Manispaa kwa ujumla iko pamoja nao na
itaendelea kushirikiana nao kwa mazuri na changamoto yeyote katika makao hayo
na wasisite kutoa taarifa pale wanapokuwa
na tatizo lolote.
“Nimmefurahishwa sana na huduma
mnazowapatia watoto wetu, kwakweli mnastahili pongezi kubwa ni wachache wenye
moyo kama wenu wa kuwasaidiahawa watoto, msikkate tamaa endeleeni na malezi
bora mwenyezi mungu atawabariki sana chukueni hiki kidogo tulichowaletea ikiwa
ni sehemu yetu ya kusherekea mwaka mpya na watoto wetu wajisikie huru na Amani badala
ya kuwa wapweke”Amesema
DC Chonjo.
Pia
amempongeza mlezi wa kituo hicho, Sister Palagia Maria, kwa kuwa na malezi
mazuri kwa watoto hao wanaoletwa kwenye Makao hayo wakiwa katika mazingira
hatarishi.
Aidha Mkurugenzi wa Manispaa ya
Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema kuwa huo ni mwendelezo wa ahadi zilizotolewa
na Mkuu wa Wilaya kwa kushrikiana vyema na Uongozi wa Manispaa ya Morogoro huku
akisema kuwa tayari baadhi ya ahadi
zimekwisha tekelezwa na zawadi nyingine kutoka kwa wahisani hivyo amemtaka
mlezi wa Makao hayo waendelee na moyo wa kuwasaidia watoto hao hadi pale watakapo pata mwangaza
wa maisha yao.
“Watoto niwaombe msome sana
mkizingatia hakuna urithi Zaidi ya elimu, Serikali ya awamu ya tano chini ya
Mhe. Rais Dkt. John Magufuli imewekka mpango wa elimu bila malipo msome sana
ili nayi baadae muweze kuwa na masiha mazuri na kuendesha familia zenu” Amesema
Sheilla.
Naye, Mlezi wa Makao hayo,
Sister Palagia Maria, amemshukuru Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi ikiwamo Ustawi
wa Jamii kwa kuwa karibu nao huku akiwataka wasikate tamaa kwani wao
wanategemea pia misaada kutoka kwa wahisani.
Mbali na kutoa chakula pamoja na
Vinywaji katika Makao ya Mgolole, Mkurugenzi Sheilla amepata nafasi ya
kutembele kituo cha kulelea Wazee wasiojiweza cha Funga Funga kilichopo Manispaa ya Morogoro na kutoa zawadi ya TV
Flat Screen na king’amuzi cha Star Times vyenye thamani ya Shilingi Laki 7.
Amesema lengo la kutoa Tv hiyo
ni kuwafanya Wazee hao waweze kuangalia mambo mbali mbali ya maendeleo
yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John
Magufuli.
Kwa upande wake Afisa Mfawidhi Kituo
cha Funga Funga, Bi Yolanda Komba,amemshukuru Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na
Idaraya Ustawi wa Jamii kwa kuwa karibu na kuwasaidia katika huduma mbali mabli
ikiwamo kuwapatia msaada na kuwajali wazee hao wenye mahitaji muhimu hivyo anamtakia kazi
njema katika kutekeleza majukumu yake na kuanza mwaka mpya kwa mafanikio zaidi.
Naye Mwenyekiti wa Wazee hao,
Mzee Joseph Kaniki, ameushukuru Uongozi wa Manispaa ya Morogoro kwa kutekeleza
akile walichokiomba huku akizidi kumuombea Mhe. Rais Magufuli afya njema ili
aweze kuiongoza vyema Tanzana katika kufikia maendeleo hususani uchumi wa Kati
na Viwanda.
Post a Comment