Header Ads

Mbunge Segerea afanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Ilani ya CCM katika Jambo lake




























Jumanne* ya leo tarehe 19/02/2019 niliambatana na wajumbe wa halmashauri kuu ya Jimbo la segerea katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kama sehemu ya usimamizi wa utekelezaji wa ILANI ya Chama cha Mapinduzi katika kata za Minazi mirefu, Kiwalani, Kipawa na Kinyerezi jimboni kwetu Segerea.

*Kata ya M/mirefu* tumekagua ujenzi wa barabara na ujenzi wa soko la Migombani
*Kata ya Kiwalani* tumekagua ujenzi wa barabara za lami na mifereji, ujenzi wa soko la Bombom Gezaulole na vyoo vilivyojengwa na fedha ya mfuko wa jimbo  katika shule za Bwawani na Muungano.


*Kata ya Kipawa* tumekagua barabara ya Airport - Karakata, upanuzi wa zahanati ya Kipawa na geti la shule ya sekondari Ilala lililojengwa na mfuko wa jimbo.


*Kata ya Kinyerezi* tumetembelea kivuko kilichojengwa na mfuko wa jimbo, soko la Kinyerezi lanaloendelea kujengwa na madarasa matatu yaliyojengwa na fedha ya mfuko wa jimbo katika shule ya msingi Kinyerezi Jica.

Kwa niaba ya wananchi wa jimbo la segerea naishukuru sana serikali yetu chini ya usimamizi mahiri wa raisi wetu Mh. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuelekeza fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo jimboni kwetu.


Pia nawashukuru watendaji wote wa serikali kwa usimamizi mzuri lakini pia wakandarasi kwa kazi nzuri wanazofanya! Nawaomba sana muikamilishe miradi ambayo haijakamilika kwa wakati kama mlivyotuahidi!

Fedha takribani bilioni 3 zimekwishatumika katika miradi tuliyopitia Leo! Tunashukuru sana! Nawaomba wananchi wenzangu tuwe wazalendo wa kuitunza miradi hii ili ikawe alama kwa kizazi kijacho!



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.