Header Ads

Diwani Mburahati aelezea alivyotekeleza Ilani ya CCM katika Kata yake




ELIMU.
Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuboresha,  kuimarisha na hata kupanua Elimu ya Awali hadi Chuo Kikuu kwa lengo la kuhakikisha kuwa Elimu katika ngazi zote inakuwa na ubora unaostahili ili kuwawezesha Vijana na makundi mengine kumudu ushindani wa Soko la Ajira ambalo Wigo wake umepanuka. Hii yote inatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.

Kata ya Mburahati ina shule 4 za Msingi na Moja ya Sekondari (zote ni za Serikali ) zipo shule zingine ambazo ni za awali zinamilikiwa na Watu wa Binafsi.

Mimi Mhe. YUSUPH OMARY YENGA Diwani wa Kata ya Mburahati katika kutekeleza Agizo hili la Serikali ya Awamu ya Tano ya Jemedari Mhe. Raisi Dkt John Pombe Joseph Magufuli tumeendelea kuhakikisha kuwa usemi wa Elimu bure unatekelezwa kuanzia ngazi ya shule ya Msingi hadi Kidato cha Nne, hakuna Mwanafunzi anayelipa Ada kwa ngazi hizo za Elimu kwa shule hizi za Serikali zilizopo ndani ya Kata yetu ya Mburahati.




Shule yetu ya Sekondari ilikuwa ina changamoto ya Majengo kwa Wananfunzi wetu kwani walikuwa wanalazimika kupeana zamu kutumia madarasa hayo kwa maana ya wengine kutumia Asubuhi - Mchana na wengine mpaka Jioni. Kwa kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano ya Jemedari Mhe. Raisi Dkt John Pombe Joseph Magufuli nimefanikiwa kabisa kutatua tatizo hilo la Majengo ya madarasa kwa kuhakikisha kuwa jengo la Ghorofa la Sekondari hiyo linakamilika haraka. Jengo lmekamilika muda mrefu na wanafunzi wananendelea kutumia jengo hilo.

Pia niwaombe wazazi wote tuhakikishe kuwa tunakuwa karibu na watoto wetu katika kuhakikisha kuwa tunafuatilia Maendeleo yao kwa kufika shuleni na kuonana na Walimu...

Mwisho Kabisa niishukuru Serikali ya Awamu ya Tano ya Kiongozi wetu mtetezi wa Wanyonge Mhe. Raisi Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa jinsi anavyowajali Wananchi wote bila kubagua.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.