Header Ads

Kumbilamoto agawa vyakula kwa Wajane Vingunguti.






 NAIBU Meya wa  Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto, amegawa vyakula kwa Wajane Wa Vingunguti baada ya mkutano mfupi wa  semina juu ya upatikanaji wa  Mikopo ya uwezeshaji kiuchumi.



Akizungumza na Waandishi Wa habari, amesema vyakula hivyo vitawasaidia kujikimu kwani kundi hilo la  Wajane miongoni mwao hawana tegemezi hivyo kupelekea baadhi ya huduma muhimu za kijamii kutopa.

 Amesema vyakula hivyo ni moja ya ahadi kutoka kwa wadau wakubwa wa  Maendeleo kutoka Kampuni ya Primiamu Agro Limited iliyoko Kata ya Vingunguti inayojishughulisha na uuzaji wa  Mbolea hapa nchini.

Aidha, amesema kikao cha Leo licha ya mgao huo wa  vyakula lakini agenda kubwa ilikuwa  ni pamoja na kuwakutanisha Wajane hao na Afisa Vijana Wa Manispaa ya Ilala ili kutoa Elimu ya mikopo.

" Napenda kutoa pongezi za dhati kwa ndugu zangu wa  Agro, wameonesha nia ya dhati ya kushirikiana na Serikali kwani walichokitoa leo  kimewafanya Wajane Hawa kuona Serikali inawajali na kuwathamini, hivyo mungu azidi kuwapngezea uzalishaji ili Siku nyingine mtoe zaidi ya hiki" Amesema Kumbilamoto.

Hata hivyo, Kumbilamoto, amesema Ilala ipo  salama chini ya DC Mjema na uongozi mzima Wa Manispaa, hivyo wamawakaribisha wawekezaji wengi zaidi ili Ushirikiano uwe bora katika kuiletea Maendeleo Wilaya hiyo.

 Pia amesema kuwa, licha ya kusaidia huduma ya chakula bado kuna huduma nyingine mbali mbali zinahitaji kusaidiwa kama vile Shule, huduma za Afya , Michezo na utamaduni katika kufikia uchumi Wa kati.

Katika hatua nyingine, Leo DC Mjema amekabidhiwa jumla ya Mifuko 100 ya Saruji na Taasisi ya Elimu ya Brothers Academy na mifuko hiyo kuelekezwa katika ukarabati wa  Shule ya Sekondari Vingunguti.

Ikumbukwe kwamba Kampuni ya Primium Agro imekuwa ikitoa misaada mbali mbali katika kusaidiana na Serikali kufikia malengo ikiwamo kutoa baadhi ya Vifaa Hospitali ya Mnyamani, Kuhudumia vyakula mashileni na kutengenezaji wa  Madawati ..

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.