Dc Mjema awataka Scout Hapa nchini kujihusisha na Kilimo kuelekea Tanzania ya Viwanda.
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amewataka Scout kujihusisha na kilimo ili kuzidi kujiimarisha kiuchumi.
Hayo ameyasema juzi katika kusherekea Siku ya kuzaliwa kwa Muasisi wa Scout Duniani.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema licha ya kujihusisha na kukuza maadili kwa Vijana wa Tanzania lakini wanataliwa kujikita katika kilimo kujiimarisha kiuchumi na kufanya chama hicho kizidi kuwalea Vijana wengi hapa nchini.
Amesema anatambua Majukumu mazito waliyo nayo kwani wanapokea Vijana wengi lakini kuna changamoto za kiuchumi ambapo wakijikita katika kilimo kutawasaidia sana.
Amesema anaamini Scout wana mchango mkubwa sana hapa nchini katika kuwalea Vijana kwenye maadili mema. .
Amesema atawapatia Ardhi Chanika ili waweze kuanzisha kilimo ili kuendana na Sera ya Mh Rais JPM ya Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati.
" Yote mliyosema nimeyapokea najua hizo changamoto zenu zina majibu lakini naanza na hili la kuwapatia Ardhi Chanika kwa ajili ya kuanza kilimo ili muweze kujiendesha zaidi katika kukidhi mahitaji yenu" Alisema DC Mjema.
Pia amesema imani yake kwamba kulingana na dhamira ya kuwafikia watu Milioni 3 lakini watawafikia zaidi ya hapo kwani anatambua ni kwa jinsi gani chama cha Scout hapa nchini kilivyojikita katika shughuli mbali mbali za kiutendaji.
" Nawapongeza sana Scout kwani kila shughuli utawakuta uwanjani wapo, shughuli za Kiserikali wapo hii inaonesha taswira nzuri ya kwamba chama hiki ndio Msingi wa malezi bora kwa Vijana wetu wa Kitanzania" Aliongeza DC Mjema.
Katika hatua nyingine , DC Mjema amewataka Scout kushiriki katika usafi wa Mazingira kwa kufanya usafi maeneo ambayo watayachagua kwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Amesema usafi ndio kila kitu hivyo pasipo na usafi hakuna Mazingira mazuri kwa Jamii.
Amewataka Viongozi kuchukua nafasi hiyo kuhakikisha kila maeneo yaliyopo Manispaa ya ilala yawe safi.
Kuhusu zoezi la Vitambulisho vya Wajasiriamali amewataka watendaji wasikae ofisini watoke nje kuviuza kwani bado wapo watu wengi hawajafikiwa na huduma hiyo.
Amesema hilo ni zoezi la Rais JPM hivyo watendaji wasisubiri DC au DAS waje nao wanatakiwa kutoka nje na kwenda katika maeneo yenye mkusanyiko walipo wafanya Biashara.
Post a Comment