DAS Ilala awashukia Watendaji Kata, atoa agizo kuhakikisha Vitambulisho vya Wajasiriamali vinakwisha
KATIBU Tawala Wilaya ya Ilala, Sheila Edward Lukuba, amewataka Watendaji wa Kata kuacha kukaa Ofisi badala yake watoke nje kuwapatia Wajasiriamali vitambulisho.
Hayo ameyasema Leo Mara baada ya ziara ya kushtukiza ya kukagua mwenendo Wa ugawaji Vitambulisho unavyokwenda katika Wilaya ya Ilala.
Akizungumza mapema Leo, amesema huu ni wakati Wa Watendaji kuacha kazi kufanya kazi na sio kukaa ofisini kitu ambacho hakitawasaidia kufanikisha zoezi hilo.
Amesema katika Wilaya yake hii ni awamu ya Tatu kugawa lakini cha kushangaza bado zoezi hilo linasua sua.
" Hili ni zoezi la Kitaifa, tufanye kazi kwa bidii hata nyie Watendaji hebu tokeni nje angalau mtafute sehemu ya mkusanyiko mnaweza kuviuza huku mkiwa elimisha Watu kuhusu umuhimu Wa Kitambulisho hicho na adhma ya Rais John Magufuli kuwatambua wao kama kundi muhimu katika kuelekea uchumi wa kati"Amesema DAS.
Pia amewataka Watendaji kuwashirikisha Wenye Viti wa Serikali za Mitaa pamoja na Maafisa Biashara wa Kata ili kurahisha zoezi hilo.
" Watendaji na Wenye Viti, hebu tujitoleeni kumsaidia Rais, mtambue hili ni zoezi la Kitaifa na Dar Es Salaam ndio kitovu kinacho angaliwa sana, sasa kama mtashindwa tutatia aibu na utendaji wetu hautakuwa salama, sisi tumetoka na nyie mtoke" Amesisitizia DAS.
Amewataka Watendaji wajitoe na kutosubiria posho.
Pia amesema kama Mtendaji Kata yake vipi Vitambulisho apeke kata nyingine ambao wana uhaba navyo.
Miongoni mwa Kata zilizofikiwa na zoezi hilo la ukaguzi ni pamona na Kata Ya Ukonga, Kiwalani pamoja na Kata ya Vingunguti.
Katika Kata ya Ukonga, awamu ya kwanza walipatiwa Vitambulisho 140 na kufanikiwa kuvimaliza na awamu hii ya tatu walipewa 500 mpaka sasa wamesha vitoa 64, halikadharika kata ya Kiwalani walipewa 500 na kugawa 27 na kata ya Vingunguti walipewa 500 wamegawa 86.
Post a Comment