Header Ads

Mkurugenzi Ilala aelezea jinsi mradi wa Hospitali ya Wilaya unavyoendelea.





MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mh Jumanne Shauri, amesema mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Ilala ulioko Kata ya Kivule umeanza rasmi na tayari mafundi wameshaanza kazi.

Akizungumza na Waandishi Wa Habari, Mkurugenzi Shauri, amesema mradi huo mpaka ukamilike utagharimu Shilingi Bilioni 7.5 ambapo mpaka sasa wameingiziwa kiasi cha Shilingi bilioni 1.5 kutoka Wizarani.

 Aidha amesema mradi huo wa Hospitali utakuwa  na Malengo 7. Miongoni Mwa Majengo  hayo ni pamoja na Jengo la  Ufuaji, X- Ray, Maabara, Madawa, Maternity ward, pamoja na Wagonjwa wa nje ( OPD).

 Amesema kuwa ujenzi huo umeanza 18 February unatarajia kumalizika Juni 30, 2019. " Tunaishukuru sana Serikali kuu  kwa kutuletea mradi huu kwani utapunguza idadi ya wagonjwa katika Vituo vyetu vya Afya na Zahanati" Amesema Shauri.

 Mbali na hapo , amesema wataongeza ulinzi katika eneo hilo na kufunga CCTV Camera pamoja na kufunga Taa  kubwa za Sola ili kuweza kutoa nafasi kwa wajenzi kufanya kazi usiku na mchana.


Naye Kaimu wa Kamati ya Fedha na Utawala, na Diwani wa Kata ya Segerea, Manase John Mjema, ameaema  madhumuni ya kutembelea Jengo hilo la  Hospitali ni kuangalia pesa za mra zinavyotumika.

Amesema kukamilika kwa Hospitali hiyo kutapunguza msongamano wa Wagonjwa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.