Header Ads

DC MJEMA AWATAKA WATENDAJI KWENDA NA KASI YA JPM















MKUU wa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema amewataka watendaji wa Manispaa ya Ilala kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Ilala.

Mjema aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam  katika kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekekezaji wa Ilani cha chama cha Mapinduzi CCM kuanzia Januari 2018 hadi Disemba 2018.

"Dhamana tulizopewa siyo kwa ajili yetu bali ni kwa ajili ya wananchi. Rais wetu ana matumaini makubwa kutoka kwetu kwamba tutawajibika katika majukumu yetu ili kuleta maendeleleo na kuifikia ndoto yake ya kuinua hali ya maisha ya watanzania "alisema Mjema.

Alisema ili Wilaya yetu iweze kusonga mbele  na Tanzania ifikie uchumi wa Kati  kila mmoja anatakiwa kuwajibika kumsaidia Rais John Magufuli.

Alisema, mtakumbuka mwaka jana nilifanya ziara katika kata zote 36 kusikiliza kero za wananchi na kukagua miradi ya maendeleo. Kazi hiyo nitaendelea nayo na Mkurugenzi wangu kupita kata kwa kata hadi mitaa yote ili tumfikie kila mwana ilala.

Mjema aliwawataka wana Ilala kuwajibika katika kufanya kazi kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli .
Akielezea utekelezaji wa Ilani January hadi Desemba 2018 Kwa upande wa mipango Miji Ilala wamejipanga kuandaa leseni za makazi 6000 na kurasimisha wakazi 2800,kuandaa vibao vya kuonyesha namba za nyumba za majina ya Mtaa .

Pia  Mjema alisema Manispaa ya Ilala ina Mpango wa kuendeleza upya maeneo ya Tabata, na Segerea, kuwezesha maboresho 200 ya michoro ya mipango miji na kulekebisha na kuchapisha ramani kuonyesha majina ya mitaa.

Pia katika sekta ya afya katika kutekeleza ilani eneo limetengwa maeneo ya Buguruni Kwa Mnyamani ili kuwezesha upanuzi wa kituo cha Afya  kiweze kuwa hospitali itakayokinga na Kutibu magonjwa mbalimbali Jumla ya shilingi 306,986,076 zilitumika katika fidia wakazi waliopo eneo hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Ilala Jumanne Shauri alisema katika utekelezaji wa Ilani idara ya Ustawi wa Jamii imetekeleza ilani ya uchaguzi  kwa kutoa mikopo kwa vikundi vya watu wenye ulemavu kwa riba nafuu  pamoja na utoaji vitamburisho vya Wazee 10,000 vya Matibabu.

Shauri alisema katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020 watu 205  Wenye ulemavu walipewa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya mikopo ili kuwawezesha kuwa na nidhamu ya FEDHA na kuelekeza fedha hizo katika kuboresha maisha yao.

Aidha alisema Manispaa ya Ilala ina Mpango wa kutekeleza Mradi wa kituo cha daladala cha kisasa Kata ya Chanika eneo la Lukooni  lenye ukubwa wa ekari 5 ambalo limelipwa Fidia. Lengo ni kurahisisha usafiri wa kwenda maeneo ya kusini ya Wilayani Ilala, na jumla ya shilingi Bilioni 190,000,000 zitatumika .

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.