DC Mjema awaasa wakina Mama Wajasiriamali kuwa mbali na Viben Ten kama wanataka kufikia Malengo
MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, awataka wakina mama kama wana ndoto za kufika mbali basi waachane na Habari za kulea Vijana katika mahusiano badala yake mikopo wanayoipata wajikite katika kuongeza mitaji ili walipe kwa wakati.
Hayo ameyasema Leo wakati akifunga maonyesho ya Wajasiriamali yaliyoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Guru Planet Limited pamoja na Ushirikiano mzuri Wa Manispaa ya Ilala.
Akizungumza na Waandishi Wa habari, amesema pamoja na kuwepo changamoto mbali mbali zinazowakabili lakini Suala la kujiingiza katika mahusiano na Vijana waliochini ya rika lao maarufu kama " Vi Ben Ten" kunaweza kuchangia wakashindwa kurudisha mikopo.
Amesema kama wakina mama wakijikita katika Michezo hiyo watajikuta marejesho kurudisha ni ngumu badala yake hata malengo yake hayatimii kwa kuchunwa pesa za mikopo na Serengeti Boys.
"Tumieni fursa mliyo nayo kutoka hapo mlipo kuingia kuingia katika uchumi Wa kati, Serikali yenu inawasikiliza na inawajali sana lazima mkumbuke hiyo mikopo mnayopewa mnatakiwa kurudisha ili na wengine wapate, sasa mkiwaendekeza hao Serengeti Boys ama Viben ten mtashindwa kufikia malengo yenu" Amesema DC Mjema.
Aidha kuhusu changamoto ya Masoko, amesema watahalikisha yeye pamoja na Naibu Meya Wa Ilala wanapambana kuwapa njia na mbuni mbali mbali ili wauze bidhaa zao.
Amesema mwaka huu wapo katika mipango ya kugeuza Uwanja huo Wa Mashujaa kuwa eneo la kutangaza bidhaa za Wana Ilala na Watanzania kwa kuandika mabango yasemayo " Ingia ndani ununue bidhaa ya Mtanzania kufikia uchumi Wa kati".
Pia amemuagiza Naibu Meya Wa Manispaa ya Ilala, Mh Omary Kumbilamoto, kuhakikisha haraka sana kufanya miundombinu ya eneo hilo iwe tayari kwa ajili ya kuendesha shughuli hizo.
Aidha, amesema Ilala wapo katika kuhakikisha wanakuea na Utalii wao wa ndani ili kuisaidia Sekta ya utalii kupiga hatua huku akisema tayari slishakutana na Waziri mwenye dhamana ya Utalii, Mh Kigwangwala na walishafikia pazuri mategemeo yake ni kuona ilala inapendeza na Wajasiriamali wake wananufaika.
Pia amesema kwa kuwa Uwanja Wa ndege upo Ilala , ataongea na Meneja Wa Uwanja huo ili kuwapa nafasi wakina mama Wa ilala kuweza kutangaza bidhaa zao pale na kujiongezea kipato.
Mbali na kuomba eneo lakini amesema kuwa kwa vile Ilala kuna vikundi vingi na haviwezi vyote vikafika atahakikisha kila siku vinakwenda angalau vikundi vitano kwa kupokezana.
" Uwanja Wa ndege ni pazuri kwani mkiwa pale huyu kaweka dafu kichwani ana nengua nengua na dafu lake wageni wakishuka ni rahisi wewe kupata pesa kwani hata wao wakiona hivyo watasema Tanzania nzuri ukishuka tuu unakutana na bidhaa mbali mbali" Ameongeza DC Mjema.
Pia kuhusu mitaji amesema mpaka sasa jumla ya vikundi 68 vipo hatua ya mwisho kuingiziwa pesa ambapo vingine vitaingizwa kwa ajili ya kuhakikiwa na vile ambavyo havija jiandikisha vifuate utaratibu.
Amesema Serikali ina muwezesha yule anayewaunga mkono kwani Tanzania ya sasa inahitaji Maendeleo hivyo anawapongeza sana Guru Planet na amehakikisha atawaunga mkono kama wao walivyofanya.
Amesema watahakikisha wanawatafutia maeneo Wajasiriamali na wakina mama ili wasiwe kila mara kupigiana simu na kutumiana meseji juu ya Biashara zao jambo ambalo halitawafikisha mbali.
Amesema kuwa alishatenga maeneo ya vipaumbele watakayotakiwa wakina mama kukaa na kufanya Biashara zao, miingoni Mwa maeneo hayo ni pamoja na pembezoni Mwa daraja jipya la Salender linalojengwa, Karimjee, Jumba la makumbusho posta, Sana la Askari Posta, Ralway kwa ajili ya kupiga kambi.
Katika kuhitimisha risala yake, DC Mjema amewataka Maafisa Maendeleo wote Wa Kata katika Manispaa ya Ilala wapempelekee taarifa ya Vikundi vyote pamoja na changamoto zao.
Pia DC Mjema amewataka wale Wajasiriamali waliokatika mfumo Wa leseni TRA na Biashara zao zinayumba basi waende TRA wapewe barua na waridi katika mfumo wa wajasiriamali wadogo wadogo na kupatiwa Vitambulisho.
Naye Mkurugenzi Mkuu Mtendaji Wa Guru Planet, Nikson Josephat, amempongeza DC Mjema, Naibu Meya pamoja na Manispaa kwa ujumla kwa kujitoa kwao kufanikisha maonyesho hayo yanakamilika na kuwa na tija.
Amesema maonyesho ya mwaka huu yamekuwa tofauti na mwanzo kwani mwitiko umekuwa mzuri sana hata bidhaa zilizoletwa zimewavutia watu wengi sana.
Aidha amesema licha ya changamoto lakini mwaka huu wameweza kutengeneza nafasi za wakina mama na Wajasiriamali kuuza bidhaa na kupata maeneo tofauti na nyuma ambapo yalikuwa ni maonyesho ya kutangaza bidhaa tuu peke yake.
" Tunamshukury sana DC Mjema amekuwa karibu sana na sisi pia pongezi kwa Manispaa husususani Dada yetu Afisa Maendeleo ametupa furaha kubwa sana lakini hata kwa naibu Meya Kumbilamoto naye alishiriki kikamilifu sana tunachowaahidi tutaendelea kufanya maonyesho hya vizuri zaidi na kuimarisha vikundi vyetu ili tufikie uchumi Wa kati" Amesema Josephat
Amesema kuwa maonyesho hata mwaka huu wamefikia leongo la kuwajengea uzoefu Wajasiriamali katika kuwapatia masoko.
Post a Comment