Header Ads

Das Ilala apokea hundi ya Milioni 22 kutoka TPDC kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Kinyerezi.











 KATIBU Tawala wa  Wilaya ya Ilala, Bi Sheila Lukuba, hii Leo amepokea hundi  yenye thamani ya pesa Milioni 22 kutoka Shirika la  Mafuta la  TPDC kwa ajili ya kujenga madarasa ya Shule ya Msingi Kinyerezi.


Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya hundi  hiyo yamefanyika katika Shule ya Msingi Kinyerezi ambapo pesa hiyo imekabidhiwa kamati ya Maendeleo ya Shule.


Akizungumza na Waandishi Wa Habari, Bi Sheila, ameupongeza uongozi mzima wa  Shirika hilo na kuwataka kuwa na moyo huo huo katika kusaidia Jamii kuleta Maendeleo.

Amesema kuwa, niwakati sasa wa Mashirika mengine na wadau kugawa gawio katika mapato yao la  5% ili kumsaidia Rais Wa Tanzania katika kufikia uchumi wa  kati Wa Tanzania ya Viwanda.



Aidha amesema Wilaya ya Ilala chini ya Mkuu Wa Wilaya hiyo, Mh Sophia Mjema, wapo pamoja na wadau wote Wa Maendeleo na imeahidi kuendelea kushirikiana nayo  katika kuiletea Maendeleo Ilala.

 " Tunaupongeza uongozi Wa TPDC , huu ni ungwana na Ushirikiano bora, kama mashirika mengine yakijitolea Tanzania itaenda kwa kasi sana na kufikia ndoto ya Mh Rais wetu katika kufikia uchumi Wa kati" Amesema Das Sheila.


Amesema DC Mjema anawasalimia na anapenda wadau hivyo leo  alitakiwa awepo kama mgeni rasmi lakini kutokana na mwingiliano wa  majukumu ameona ni vyema akamwakilisha.

Pia amesema kuwa changamoto zote amezipokea na atazifanyia kazi japo  sio zote lakini watapunguza.

Ameitaka kamati ya Maendeleo kuzitumia pesa hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.

 " Natoa angalizo hizo pesa zinatafutwa kwa jasho hata nyie pia nafikiri mlipata wakati mgumu kumpata mdau, sasa thamani ya pesa hiyo iendane na ubora Wa madarasa yatakayo tengenezwa tunataka Values for Money au tumieni force Account " Ameongeza Das.

Pia amewaasa Wanafunzi kusoma kwa bidii ili wasiwaangushe wadau wanaojitolea kwa ajili yao na kufanya Taifa kuwa na wasomi wengi zaidi.

Naye Meneja Wa Mawasiliano TPDC, Marie Msellemu,  amesema pesa hiyo itumike vizuri kwani wao ni utaratibu wao kutoa gawio katika kusaidia huduma za kijamii.Pia amesema wasichoke kuwaomba msaada kwani muda na wakati wote milango ipo  wazi.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.