CUF yazidi kusambaratika , Mwenyekiti mwengine aliamsha dude atimkia CCM kuunga mkono Juhudi za Rais JPM.
CHAMA cha Wananchi CUF, kimezidi kusambaratika baada ya Leo Mwenyekiti wao kutoka Kata ya Kisukuru , Mtaa Wa Kihimbwa, Said Abdallah Mungi, kujiuzuru nyadhifa zake zote na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM..
Akizungumza na mwandishi Wa habari mapema Leo, Mwenyekiti huyo amesema kujiuzuru kwake kumetokana na mapenzi yake kwa CCM nawala hakuna mtu aliyemshawishi.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inatekeleza kile walichodhamiria. Amesema Serikali ya sasa sio ya porojo ni Serikali ya kazi hivyo anaamini ujio wake CCM ni kutokana na Sera nzuri za Chama Cha Mapinduzi.
" Nimejiunga CCM kwa mapenzi yangu, nitafanya kazi kwa moyo mmoja ili kutekeleza Ilani ya CCM katika kufanya Tanzania kufikia uchumi Wa Kati" Amesema Mungi.
Licha ya kujiuzuru nafasi hiyo ya Uwenyekiti Wa Mtaa, ikumbukwe kwamba kabla ya kujiunga na CCM, alishawahi kuwa Mwenyekiti Wa Kata ya Seif Sharifu Hamadi pamoja na kuwa Katibu Wa Tawi hilo la Seif Sharif Hamadi.
Naye Katibu wa Tawi la CCM Karume Kata ya Kisukuru , Bi Minza Zakaria Shigukuru , amesema CCM unafanya kazi na kila mtu hivyo wapo tayari kushirikiana nae kwa ajili ya kutekeleza Ilani ya CCM.
Post a Comment