Header Ads

DIWANI MBURAHATI ATOA PONGEZI KWA WANANCHI WAKE



Kipekee kabisa Ofisi ya Mheshimiwa Diwani Kata ya Mburahati inapenda kuwashukuru Wananchi wote wa Kata ya Mburahati waliojitokeza kwa wingi na wale wasiojitokeza pia katika Mkutano wa Wananchi uliyofanyika siku ya Jumapili Tarehe 10 February 2019 katika Mtaa wa Barafu eneo la Viwanja vya Darajani.

Shukrani zaidi ziwafikie wale wote waliojitokeza katika Maandalizi ya Mkutano huo. Tunawashkuru sana Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Barafu wakiongozwa na Mwenyekiti Ndg. Dickson Tungaraza pamoja na Wajumbe wake, pia Viongozi wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya Kata na Matawi yote manne pamoja na Uongozi mzima wa UVCCM Kata na Matawi yake. Nyote mlifanikisha maandalizi ya Mkutano huo.

Hakika ulikuwa ni Mkutano mzuri sana ambao kila Mwananchi alivutiwa kutokana na kile ambacho Mheshimiwa Diwani wetu Yusuph Omary Yenga alikizungumza kwa Wananchi hao na kusikiliza kero zao.

Katika maelezo yake Mheshimiwa Diwani Kata ya Mburahati aligusia katika sekta ya Miundombinu hasa Barabara, ambapo alisema kuwa kuna Mradi mkubwa wa Barabara unaoendelea katika Mtaa wa Barafu na Mtaa wa Kisiwani pia kutakuwa na uboreshaji wa mifereji katika maeneo yote ambapo Mto umepita ndani ya Kata yetu.

Katika sekta ya Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Diwani alisema kuwa kwa sasa hali ya Ulinzi na Usalama katika Kata yetu umeimarika kutokana na uwepo wa Kituo cha Polisi cha Kisasa kabisa. Hizi ni juhudi zangu mimi binafsi Diwani chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Jemedari Mhe. Raisi Dkt John Pombe Joseph Magufuli pia kwa Msaada wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na aliyekuwa RPC wa Dar es Salaam Simon Sirro (sasa ni IGP) walinisaidia upatikanaji wa Kituo hiki. Alisema Mhe. Diwani.

Upatikanaji wa Maji kwa sasa ndani ya Kata ya Mburahati ni wa kuridhisha sana. Huduma za Afya pia zimeboreshwa kwa Kiasi kikubwa kwani kwa sasa tuna Zahanati nzuri sana ndani ya Kata yetu ya Mburahati.

Swala la Mikopo ya Vikundi vya kinamama na Vijana kwani licha ya uwepo wa Vikundi hivyo mpaka sasa hakuna kikundi hata kimoja kilichopata Mkopo licha ya kuwa wamekidhi vigezo vya kupata Mikopo hiyo. Diwani alimuomba Katibu wa UWT (W) Ubungo ambaye naye pia alikuwepo katika Mkutano huo kufuatilia suala hilo haraka na kuhakikisha kuwa Vikundi hivyo vinapata Mikopo.

Mwisho ilifanyika Sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa Mheshimiwa Diwani Kata ya Mburahati Mhe. YUSUPH OMARY YENGA

Asanteni Sana Wananchi wa Kata ya Mburahati.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.