Header Ads

DC Mjema apokea Mifuko 100 ya Saruji kutoka kwa Brothers Academy.








 MKUU Wa Wilaya ya Ilala,  Mh Sophia Mjema, leo amepokea Jumla ya Mifuko 100 ya Saruji kutoka kwa Wadau Wa Elimu Tanzania, Brothers Academy.



Hafla hiyo fupi ya makabidhiano hayo ya Saruji, yamefanyika leo  kwenye Ofisi ya Mkuu Wa Wilaya, ambapo ugeni huo uliambatana na Naibu Meya Wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto, pamoja na Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilala.

Akizungumza na Waandishi Wa habari, DC Mjema amewashukuru wadau hao akisema hicho kidogo kwao ni kikubwa kwani kitasaidia katika Ujenzi Wa Madarasa unaoendelea katika Manispaa hiyo upande Wa Shule za Sekondari.

 Amesema bado wana uhaba Wa madarasa hivyo amewaomba wadau wengine wajitolee ili kuwawekea mazingira mazuri na rafiki kwa Wanafunzi waliopo Wilaya yake na Tanzania kwa ujumla.

" Serikali imetoa Elimu bure, hivyo ni wakati sasa wadau kusaidia Serikali yao kwani tukifanya hivyo tutazalisha wasomi wengi  kufikia uchumi Wa Wa Viwanda" Amesema DC Mjema.

Kwa upande Wa Naibu Meya, Omary Kumbilamoto, amempongeza Mkurugenzi Wa Brothers Academy, kwa moyo wake wa kumuunga mkono Mh Rais John Magufuli katika mpango wake wa  Elimu bure.

" Tunashukuru sana , Hawa ndio wadau wenye  uchungu na Maendeleo ya Elimu Manispaa yetu, sasa kama kuna wengine wajitokeze kama alivyosema mama yangu mpendwa Mh Sophia Mjema tunaupungufu kweli Wa madarasa ukizingatia mwaka huu tulifaulisha wanafunzi 15126 kwenda Sekondari lakini wanafunzi 6000 hawajawasili Shuleni hivyo misaada kama hii inatusaidia sana" Amesema Kumbilamoto.

Naye Mkurugenzi wa  Brothers Academy, Robert Rwezaula, amesema wametoa msaada huo wa Mifuko ya Saruji kusaidia Elimu Manispaa ya Ilala.

 Amesema japo  ni kidogo lakini wanatambua kazi kubwa wanayoifanya Uongozi Wa Manispaa ukiongozwa na Mkuu Wa Wilaya, Mh Sophia Mjema ni kubwa na matokeo yake yanaonekana.

" DC Mjema anafanya kazi kubwa ukiangalia katika matokea Manispaa ya Ilala inafanya  vyema sana katika Sekta ya Elimu " Amesema Rwezaula.





No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.