Header Ads

WADAU WA MTO PANGANI KUIMARISHA MATUMIZI YAKE SAME





Pangani Basin wakishirikiana na TAHA na Wilaya ya Same wameitisha kikao cha wadau wa mto pangani ili kujadili matumizi endelevu na yenye tija ya mto huo.

Wadau hao waliojumuisha wakulima,  wafugaji, wavuvi, jumuia ya watumia maji, tanesco nyumba ya mungu, halmashauri ya Same, viongozi wa vijiji na kata. Wakubaliana kila mdau kuutumia mto huo kwa faida yake na ya wengine.

Waweka mkakati wa kutunza mazingira ya mto, kuhuisha jumuiza za watumia maji, kutengeneza mpango mahsusi wa namna ya kuuboresha, kuongeza mifereji ya umwagiliaji, kuimarisha maeneo ya malisho na mengine.

Wakulima/wafugaji wako tayari kuchangia maboresho.
DC Same Mh. Rosemary Senyamule asisitiza swala la viongozi ngazi zote kusimamia sheria na kuchukua hatua stahiki ili wale wasibadilika wawajibishwe.

" Sisi Wilaya ya Same tumejipanga kuutumia mtuo huo kama chanzo kikubwa cha uchumi kwa mapato ya  Wilaya na mtu mmoja mmoja. Hivyo kwetu kuutunza ni wajibu muhimu" alisema DC Huyo.


Meneja wa bonde la pangani awaeleza wadau athari za kuuharibu mto huo. Na mipango waliyonayo ili kuuendeleza.

Kamati ndogo yaundwa kusimamia utekelezaji wa maazimio.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.