DC Mjema apokea mradi wa Kisima wenye thamani ya Milioni 41 kutoka Lion Klabu.
MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, amepokea Maradi wa Kisima wenye thamani ya Shilingi Milioni 41 kutoka kwa Taasisi ya Lion Klabu leo.
Hafla hiyo ya makabidhiano ya mradi huo Wa Kisima imefanyika Kata ya Kiwalani ambapo mradi huo unaweza kuhudumia Shule nne kwa pamoja ikiwamo, Shule ya Msingi Kiwalani, Mwale, Yombo pamoja na Shule ya Umoja.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, DC Mjema, ameupongeza Uongozi wa Lion Klabu kwa kujitolea huduma hiyo katika kufanikisha Wanafunzi wanapata Maji safi na Salama. Pia amesema hatarajii kuona mradi huo unatumika kibiashara na watu Wa nje , hivyo ameitaka Kamati ya Shule kuwa makini kuona huduma hizo zinawafikia walengwa.
Amesema kwa sasa Kiwalani haina shida ya Maji, ifikapo mwisho Wa mwezi huu, mitaa yote itakuwa na Maji.
" Niseme kuwa huu ni uzalendo Wa hali ya juu sana, tunawashukuru sana Lion Klabu mmetupatia mradi mzuri sana ambao utasaidia kuwapa watoto wetu Maji safi na salama, tunawaahidi kwamba Serikali yetu itambeba yule ambaye anatuunga mkono kama mlivyo fanya tupo pamoja " Amesema DC Mjema.
Katika hatua nyingine, ameumba Uongozi wa Lion Klabu Tanzanite, kuendelea kuitumia Sera yao ya kutembelea kila Mara na kuhakikisha mradi huo unakuwa salama na wao kupitia Kamati ya Maendeleo ya Shule zote nne kuwa na mipango thabiti ya kulinda mradi huo.
Pia amesema kwa wale Vishoka na wapiga dili muda wake umekwisha kwani awali walikuwa wakichimba visima kuwauzia watu Maji na sasa Serikali imeliona hilo inasimamia yenyewe ili kuongeza pato la nchi kupitia Sekta ya Maji.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mama Thomas , ambaye pia ni Afisa Elimu Msingi Manispaa, amesema mradi huo uthaminiwe na utumike kwa matumizi maalumu.
Pia amesema zipo changamoto nyingi kwahyo wadau wajitokeze kuwaunga mkono. Kwa upande wa Gavana Wa Lion Klabu, Mustafa Kudrati, amesema hiyo ni mradi wao wa 24 katika kuwafikia Wanafunzi katika ujenzi Wa Visima.
Amesema Kisima hicho kimechimbwa Mita 100 kushuka chini na kinauwezo wa kubeba Lita Elfu 17.
Pia Kisima hicho kitahudumia jumla ya Wanafunzi 4678 ambapo kati ya hao, Walimu 103 Wanawake na Walimu 9 wakiume. Katika kuhitimisha hafla hiyo, DC Mjema, amewataka Wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuepuka kujiingiza katika magenge hatarishi ikiwamo uvutaji bangi, Dawa za kulevya n.k.
Pia amewaomba watoto wa kike kutojihusisha na mapenzi kwani kwa kufanya hivyo watazaa mapema na kukatisha ndoto zao." Mmesikia wanangu mwanaume akikuita unatakiwa umjibu ' No Babies' sawa hiyo ndiyo iwe kauli mbiu yenu mtafika mbali" Ameongeza DC Mjema.
Post a Comment