Mbunge jimbo la Mbagala mh.Issa Mangungu Leo alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano Mkuu Ccm kata ya kiburugwa
Katika mkutano huo Maalum uliohudhuriwa na wajumbe wengi kwenye kata hiyo umekwenda kuweka historia kubwa kabisa ya mapinduzi ya kijani kwenye kata hiyo ambayo kwa mid a mrefu imekuwa ikijulikana kama Pemba ndogo lakini kwa juhudi kubwa ya Kazi inayofanywa na chama cha mapinduzi kwenye nchi hii na kwenye jimbo na kata kwa ujumla katika utekelezaji Wa ilani ya chama wanakiburugwa kwa umoja wao sasa wameamua kukiunga mkono chama cha mapinduzi hayo yalisemwa na Mwenyekiti Wa Ccm Wa kata hiyo ndg *Ndunguru*
Na pale alipopata nafasi ya kusema neno mgeni rasmi Katika mkutano huo mh Mbunge nae aliwaomba sana wanakiburugwa kwa umoja wao sasa waseme *kutawaliwa basi* hakuna sababu tena ya kuendelea kutawaliwa kwanza kwenye mitaa *2019* na baadae kwenye chaguzi kuu kuhakikisha Kiburugwa sasa inakuwa ni ya kijani mkiamua wana Kiburugwa hili linawezekana sana naomba sasa muanze kuamua kwa vitendo muanze kunionesha mnaanza mapinduzi hayo kwenye chaguzi za mitaa *2019*
Mwisho kabisa wanakiburugwa kupitia kwa Katibu kata wao walimhakikishia mh Mbunge wamedhamiri na wameamua sasa kuleta heshima ya chama cha mapinduzi kata ya Kiburugwa
Post a Comment