UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI ( CCM ) 2015 - 2020 KATA YA MBURAHATI
MIUNDOMBINU.
Katika Kata yetu ya Mburahati kuna Mradi wa Barabara katika Mitaa Miwili ambayo ni Barafu na Kisiwani (kwa Awamu ya Kwanza).Barabara hizo zinajengwa na Mkandarasi CRJE EAST AFRICA COMPANY LIMITED.
Katika kuhakikisha kuwa Kata ya Mburahati inakuwa Kata ya mfano miongoni mwa Kata 14 zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kuwa na miundombinu ya kisasa kwa maana ya Barabara, Mhe. Diwani wa Kata ya Mburahati Mhe. YUSUPH OMARY YENGA chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Jemedari Mhe. Raisi Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.... amekuwa akipambana Usiku na Mchana katika kuhakikisha kuwa Mburahati inapata miundombinu ya kisasa.
Katika kufanikisha hilo, kwa sasa watu wote tutakuwa mashahidi kwa kile kinachoendelea katika Mtaa wa Barafu ambapo kuna Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami. Barabara hyo imeanzia kona ya Kituo cha Daladala Msikitini/ Ceda Bar/kijiwe cha Bodaboda, mbele kidogo Barabara imegawanyika ambapo moja inanyoosha kwenda Mburahati Sekondari hadi Msikiti wa kwa Sheikh Mbukuzi, pia Barabara ingine inapita kwa upande wa nyuma (kwa Jadi/Mama Kabata) ambayo inapita hadi Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Barafu inaenda hadi kwa Shebe na kuishia karibia na njia ya kutokea Magomen Mtambani (awamu ya kwanza).
Hakika kwa sasa Mburahati inapendeza, licha ya kwamba bado Barabara haijakamilika lakini mwanga wa itakavyokuwa unaonekana. Ujenzi utaendelea pia kwa Mtaa wa Kisiwani mara tu taratibu zikapokamilika.
Mhe. Diwani wa Kata ya Mburahati Mhe. YUSUPH OMARY YENGA anatoa Rai kwa Wananchi wote kuhakikisha kuwa Miundombinu hiyo inatunzwa vizuri katika kuleta manufaa kwa watu wote ambapo Ajira mbalimbali zitazalishwa kutokana na uboreshaji huu wa miundombinu ya Barabara, pia itarahisisha upatikanaji wa Huduma Bora za Usafiri na kwa wakati katika kipindi chote cha Mwaka..
HONGERA SANA MHE. DIWANI WA KATA YA MBURAHATI MHE. YUSUPH OMARY YENGA hakika Juhudi zako zinaonekana
#ng'aramburahating'ara
Post a Comment