DIWANI KATA YA MBURAHATI AKABIDHI CHOO CHA KISASA KWA WAKAZI WAKE.
DIWANI wa Kata ya Mburahati, Mh: Yusuph Omary Yenga, hivi karibuni amekabidhi mradi Wa Choo cha Kisasa kwa wakazi wake ikiwa na lengo la kuhifadhi Mazingira katika Kata yake.
Hii ni mipango na harakati za Diwani huyo mwenye moyo Wa kipekee katika kuleta Maendeleo ndani ya Kata ya Mburahati.
Ikumbukwe kwamba Choo hicho cha Kisasa kabisa cha Umma ambacho kipo ndani ya Kata ya Mburahati Mtaa wa Mburahati Barafu, kitakuwa Mkombozi Mkubwa sana hasa katika swala zima la Uhifadhi wa Mazingira kwa kutokukojoa Ovyo katika maeneo ya Viwanja vya Mpira.
Kukamilika kwa Choo hicho kwa asilimia kubwa kitakuwa kinatoa Huduma kwa Jinsia zote mbili, ya kike na jinsi ya kiume.
Mradi wa choo hicho cha kisasa utakuwa na tundu tatu za Choo pamoja na bafu moja.
Hii inastahili pongezi kubwa sana kwa Diwani Yenga katika kuhakikisha Kata yake na wananchi wake wanapata Maendeleo katika kuelekea uchumi Wa kati.
Akizungumza na tovuti ya chombohuru huru, Diwani Omary Yenga , amsema yupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wake hivyo yote anayoyafanya ni kulipa fadhila kwa wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.
" Haya yote nayafanya ili wananchi wangu wasipate shida, niliwaahidi sasa niutendaji kama Ilani ya chama chetu dume cha CCM ilivyoelekeza"Amesema Diwani Yenga.
Post a Comment