RC Makonda kuongeza siku tano zoezi la wakina mama
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda ameongeza siku tano zoezi la kuwapatia msaada wa kisheria wakina mama waliotelekezwa na waume zao,ambapo amesema kwanzia wiki ijayo wataanza kusikilizwa wakina baba wanaolalamikiwa pamoja na kuwasikiliza wakina mama waliobakia na kuwataka wanaume watakaoitwa wafike bila kukosa ili kuepusha kutajwa majina yao hadharani.
Rc Makonda amesema wanaume watakaopewa wito wa kufika ofisini kwake wasikaidi kwani atakayeshindwa kufika jina lake litatajwa hadharani, na pia amewapongeza wakina baba waliokubali wito na kusema kuwa kwanzia wiki ijayo wakina baba wanaolalamikiwa wataanza kufika kwa ajili ya upatanishi.
"Wakina baba wanaolalamikiwa waliopewa wito wataanza kufika kwanzia jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya upatanishi na wale watakaokaidi tutataja majina yao hadharani hivyo wakina baba watakaokaidi kuja kwa ajili ya kupatanishwa nitawatangaza majina yao hadharani"Amesema Makonda.
Aidha amesema wapo watu wanaobeza zoezi hilo katika mitandao na kuona ni jambo la Faragha,ambapo amesema lengo la zoezi hilo siyo kumuumbua mtu bali ni kutafuta haki ya kila mtoto na kuondokana na watoto omba omba walioko mitaani.
"Nyie mlioko nyumbani mnahaki ya kubeza hili zoezi nmna haki ya kuandika mnachoandika lakini mimi namtazama mama anayeteseka, kwaiyo waache waseme wanachokisema lakini mimi furaha yangu ni amani ya watoto na kina mama wanaoteseka"Amesema Rc Makonda.
Amesema zoezi hilo lina faida kwa wakinamama wote hata walioko kwenye ndoa kwani litasaidia kuwapatia haki watoto wote na kusaidia watoto kufahamika katika familiya na kubainisha kuwa hii itasaidia kupunguza wakina dada wanaowaza kutoa mimba ama kutupa watoto wachanga.
Pia amewaasa wakina mama na wanawake wote wa mkoa huo kutumia kinga wakati wanapofanya tendo la ndoa ili kupunguza kasi ya Ugonjwa wa UKIMWI kwani kwa kipindi kifupi ugonjwa huo umeongezeka kwa asilimia 45% kwa watoto wenye umri chini ya miaka 24.
"Tunataka katika mkoa huu kina dada wasiwaze kutoa mimba, wasiwaze kutupa kichanga na wanaume wanaopanga kuwapa mimba mwanamke kama ajajipanga aogope kama ilivyo kubaka"Amesema.
Kwa upande wao kina Mama waliofika kupatiwa huduama wamemshukuru Rc Makonda kwa kutambua na kuona kilio chao ambapo wameshangazwa na watu wanaobeza zoezi hilo ambalo wanaona limewasaidia kupata haki zao na za watoto wao.
Tokea kuanza kwa zoezi la kuwasikiliza wakina mama waliotelekezwa na kupatiwa msaada wa kisheria zaidi ya kina mama 10,000 wamefika kupata huduma na kati yao wanawake 4,000 wamesikilizwa na Familiya 205, wamekubali kwa maandishi kuwahudumia watoto wao na wengine 21
Post a Comment