Header Ads

Pogba: Kuitazama Man City ilikuwa kama kifo


Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amesema kitendo cha kuwatazama wapinzani wao Manchester City wakibeba ubingwa mbele yao ilikuwa ni sawa na kufa ndio maana walijitahidi kuhakikisha hilo halitokei.

"Sikutaka kupoteza dhidi ya Man City kwasababu walipotufunga msimu uliopita maumivu yake bado nayakumbuka hivyo sikutaka kuona tunapoteza tena, pia wao kuchukua taji mbele yetu ingekuwa ni kama adhabu ya kifo kwa mashabiki wetu," amesema.

Pogba pia ameweka wazi siri iliyowafanya wakarejea mchezoni kipindi cha pili kuwa wakati wa mapumziko katika vyumba vya kubadilishia nguo waliambiana hawana cha kupoteza hivyo ni lazima watoke wakatafute ushindi na wakafanikiwa.

Pogba alifunga mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za 53 na 55 na kusawazisha mabao mawili ya Man City yaliyofungwa kipindi cha kwanza na nahodha Vicent Kompany dakika ya 25 na Ilkay Gundogan dakika ya 30.

Kama Man City wangeshinda jana wangeshangilia ubingwa mbele ya mashabiki na wachezaji wa Man United lakini mlinzi Chris Smalling alizima ndoto hiyo dakika ya 69 baada ya kufunga bao la tatu ambalo lilifanya mchezo huo kumalizika kwa 2-3.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.