Kocha: Sina mpango wa kumshinikiza Iniesta
Andres Iniesta
KOCHA wa Barcelona, Ernest Valverde amesema hana mpango wa kumshinikiza Andres Iniesta kubakia katika timu hiyo. Iniesta amewahi kukaririwa siku za nyuma akisema kuwa atafanya uamuzi mwishoni mwa msimu huu ikiwa kama atabakia katika timu hiyo au ataondoka.
Kiungo huyo amekuwa na Barcelona tangu mwaka 1996, ambako alijiunga na timu ya watoto na alianza kuchezea timu ya wakubwa 2001. Iniesta anadai kuwa amepokea ofa nyingi zikiwamo za kwenda kucheza soka ya kulipwa nchini China.
“Iniesta amesema kuwa atatangaza uamuzi wake hivi karibuni na nitauheshimu,” alisema Valverde. Valverde alisema hahitaji kumshinikiza au kumshawishi abaki kwa kuwa yeye mwenyewe (Iniesta) anajua anavyoubalika ndani ya klabu hiyo

Post a Comment