Header Ads

IFM imetoa msaada kwa watu wenye uhitaji


Chuo Cha Usimamizi wa Fedha IFM Tawi la Mwanza kupitia Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi umeungana na jamii kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye uhitaji maalumu.

Akiongea mara baada ya kukabidhi misaada hiyo kwenye kituo cha kupinga dhidi ya watoto majumbani (FKT) Rais wa Chuo hicho Peter Kahindi alisema lengo kubwa ni kuiasa jamii kuondokana na vitendo vya ukatili majumbani.

"Tumeguswa na watu wenye uhitaji kwani hao ndio waathirika wakubwa katika jamii hasa pale linapokuja suala la chakula, mavazi na malazi tumeona ni bora tujumuike nao karibu wasionwe wametengwa na jamii," alisema Rais Kahindi.

Rais Kahindi alitaja misaada iliyotolewa kwenye kituo hicho kuwa ni Nguo, Mchele, Magodoro, Sukari, Sabuni, Madaftari kalamu kwa ajili ya kujisomea vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 3.

Akipokea msaada huo Mwakilishi wa Kituo Asunta Ngatunga alisema ameshukuru kwani msaada huo unamchango mkubwa katika kituo hicho.

Kwa upande wake Lucy Hiza ambaye yupo kitengo cha Idara ya Uokoaji wa Watoto alisema licha ya elimu kutolewa kwenye Jamii na wazazi wa watoto bado ukatili huko juu kwa Mkoa wa Mwanza.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.