Arsenal yapewa Atletico Nusu Fainali Europa Ligi

Droo ya timu zitakazocheza hatua ya nusu fainali ya UEFA Europa League tayari imeshapangwa ambapo Arsenal itakutana na Atletico de Madrid ya Spain.
Arsenal ilifuzu kuingia hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 6-3 dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi.
Arsenal wataanzia nyumbani Aprili 26 kwa mechi ya mkondo wa kwanza kabla ya kurudiana na Atletico May 3 2018.
Mbali na Arsenal, Marseille ya Ufaransa pia imepangwa kucheza na Salzburg ya Ujerumani kucheza hatua hiyo ya rnusu fainali.

Post a Comment