Vee Money: Kwa sasa kiukweli tutabanana hapahapa
Vanessa Mdee ‘Vee Money’
MWANA-DADA anayekimbiza na albamu ya Money Mondays, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, amefunguka kuwa kutokana na maprodyuza wa video za muziki kujitambua na kuanza kutengeneza kazi nzuri, hakuna haja ya kutoka nje kwa sasa.
Akipiga stori na Showbiz Xtra, Vee ambaye ametambulisha pia video yake ya wimbo namba tisa unaopatikana kwenye albamu yake hiyo uitwao Wet aliomshirikisha G Nako, aliongeza kwamba hata akiwa na hamu ya kufanya kazi na prodyuza wa nje atahakikisha anamleta Bongo ili ashirikiane na maprodyuza wa ndani kufanya kazi.
“Kwa sasa kiukweli tutabanana hapahapa. Mambo ya kutoka nje huku maprodyuza wetu wanafanya kazi nzuri sioni kama ni kitu kizuri kwa sasa, binafsi kazi nyingi nitafanyia Bongo,” alimaliza Vee Money.

Post a Comment