Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki ametoa salamu za rambirambi kwa nchi ya Algeria baada ya ajali ya ndege ya kijeshi iliyopelekea vifo vya watu 257.
Waziri Çavuşoğlu katika mtandao wale wa twitter ameandika kuwa amesikitishwa sana na ajali hiyo iliyopelekea idadi kubwa ya vifo vya raia nchini Algeria.
Ametoa pole kwa jamaa na marafiki wote walioguswa na ajali hiyo.
Jumla ya abiria 247 na wafanyakazi 10 wamepoteza maisha katika ajali hiyo ya ndege ya jeshi.
Haijajulikana bado kama kuna mtu hata mmoja ameokoka katika ajali hiyo.
Post a Comment