Kocha Mbea City: Simba na Yanga sio timu za kutisha
Kocha wa klabu ya Mbeya City, Ramadhan Nswanzurwimo, haoni ukubwa wa timu za Yanga na Simba kwa kueleza kuwa havina utofauti wowote timu yake.
Nswazurwimo ametamka maneno hayo baada ya kichapo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Sports Xtra, Kocha huyo alisema kuwa Yanga na Simba si timu kubwa huku akieleza kuwa zote pamoja na Mbeya City ziko kwenye levo moja.
Mbali na hilo, Nswazurwino alisema utofauti wa Mbeya City na timu hizo upo katika ligi tu ambapo timu moja inafanya vizuri huku nyingine ikiwa haifanyi vizuri.
"Yanga na Simba si timu kubwa, utofauti unakuja kwenye eneo moja pekee ambapo timu moja inafanya vizuri kwenye ligi huku nyingine ikiwa haifanyi vizuri, timu zote ziko kwenye levo moja hivyo Yanga na Simba zi timu kubwa" alisema.

Post a Comment