Header Ads

KAMATI YA FEDHA MANISPAA YA MOROGORO YAPONGEZA MENEJIMENTI MANISPAA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO


KAMATI ya Fedha na Utawala Manispaa ya Morogoro imeipongeza Menejimenti ya Manispaa ya Morogoro  kwa usimamizi mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa  katika Kata mbalimbali za Manispaa hiyo.

Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala wametoa pongezi hizo hivi karibuni Oktoba 2023 katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, kwa niaba ya wajumbe amemshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuipatia Manispaa ya Morogoro  fedha nyingi sana za miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa Baraza la Madiwani kupitia Kamati zake za Kudumu litafanya kazi zake ipasavyo kuhakikisha kuwa miradi inajengwa kwa ubora uliuokusudiwa na thamani ya fedha katika miradi inaonekana.

Katika kuhitimisha Ziara hii, Mhe. Kalungwana,  amewasihi sana Wataalamu wa Manispaa ya Morogoro kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na wajenge utamaduni wa kukubali kukosolewa na kupokea ushauri wa wadau mbalimbali hususani kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Mwisho Kamati hiyo iliomba muda wa nyongeza ya kukagua miradi ya maendeleo ili kuhakikisha changamaoto zinazojitokeza katika miradi hiyo zinataturiwa kwa wakati.

Katika eneo la mradi wa Machinjio, Kamati hiyo imeshauri ujenzi huo uzingatie ubora ili uweze kuwa mradi wa mfano na wa kisasa.

Miongoni mwa miradi ambayo kamati imekagua ni ujenzi wa Jengo jipya la Shule ya Sekondari Konga Kata ya Mzinga, Jengo la Bweni la Sekondari Kilakala, Ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule Msingi Mtawala kupitia nguvu za wananchi na Diwani wao, eneo la Ujenzi wa Machinjio ya kisasa linalotarajia kutumia Milioni 150 eneo la Mkundi, Ujenzi wa Nyumba ya waalimu Shule ya Sekondari Mindu, 


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.