MANISPAA YA MOROGORO YAJIANDAA KUKABILIANA NA MVUA ZA EL-NINO
MANISPAA ya Morogoro imejipanga kukabiliana na Mvua za El- Nino zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni kwa kutenga Milioni 30 kwa ajili ya kutatua changamoto zitakazowakumba wahanga wa mafuriko.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ,Ally Machela, mara baada ya kumalizika kwa Baraza la Kawaida la Madiwani robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa.
Machela, amesema licha ya kutenga fedha hizo lakini watahakikisha maeneo yote yenye viashiria vya kukumbwa na mafuriko watahakikisha vituo vya afya na Zahanati vinakuwa na dawa za kutosha kwa wale wagonjwa watakao kuwa wameathirika na mafuriko hayo.
Aidha, amesema kuwa elimu tayari imeshatolewa katika maeneo yenye viashiria vya mafuriko huku baadhi ya wananchi zaidi ya 130 walijitokeza kuhitaji Viwanja mbadala ili kuepukana na athari hizo za Mafuriko.
"Tayari timu yetu imeshapita mitaani kutoa elimu, lakini tuliwaomba pia wahame hayo maeneo na tumepokea maombi ya wananchi 130 ambao tunatarajia kuwapatia maeneo Kiegea kwa ajili ya kujenga nyumba zao kwa bei nafuu ya skwea mita 1 kwa shilingi 3500" Amesema Machela.
Hata hivyo,amesema kwa kutumia exakaveta ya Manispaa wamejipanga kuanza kusafisha mitaro na mifereji yote katika maeneo yenye viashiria vya mafuriko kwa lengo la kuokoa na kupunguza maafa yanayoweza kujitokeza hapo baadae.
"Tunaelekea kwenye hatari ya mvua hizo,wito wangu kwa wananchi kulinda mitaro hii maana madhara yake ni mafuriko ambayo yatahatarisha maisha ya watu, tunaomba wananchi wakati tunaifukua mitaro yetu waendelee kuilinda ili kuweza kutunza na kuweza kuwezesha maji kupita kama ilivyokusudiwa"Ameongeza Machela.
Mwisho, Machela, amesema Manispaa ya Morogoro imesainia mkataba na Kampuni ya Ujenzi ya... kupitia miradi ta Tactics ambayo imelenga pia kutatua changamoto za Mifereji ya maji itakayoondoa mafuriko katikati ya Mji.
Post a Comment