Header Ads

CCM WILAYA YA MOROGORO MJINI YAPONGEZA CHUO CHA VETA MOROGORO KWA ELIMU BORA WANAYOITOA YA KUZALISHA WATAALAMU


 

CHAMA Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini  kimepongeza Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Morogoro  kwa kuendelea kutoa huduma bora wanafunzi ambao wanachukua ujuzi mbalimbali katika Chuo hicho  katika kusongesha mbele gurudumu la elimu.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma katika zira ya Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Morogoro Mjini ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo ikiwa na lengo la kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya na wafanyakazi wa Chuo hicho, Fikiri,  amesema VETA imekuwa ni Taasisi  ya mfano kwa namna inavyoendesha shughuli za elimu kwa kushirikiana kwa ukaribu na Serikali.

Aidha Fikiri ,amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa Chuo hicho na ipo tayari wakati wowote kwa ushirikiano wa kujenga taifa kwani inaamini wataalamu wengi hutengenezwa katika vyuo vya ufundi na kupata wataalamu ambao wataifikisha Tanzania katika uchumi wa Viwanda.

Vilevile amevitaka vyuo vyengine kuiga mfano wa VETA katika utoaji wa elimu lakini pia kuzingatia maeneo ya michezo kwa kuwa michezo na sanaa ni sehemu ya elimu na kwa kufanya hivyo kutawandaa vyema wanafunzi kiakili na kutengeneza ajira nyingi zaidi nje ya taaluma zao.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Morogoro, Andrew Boi, amesema kuwa watanzania waendeelee kuviamini vyuo vya ufundi stadi  kwa namna zinavyotoa elimu na kuzalisha wataalamu wazuri kwenye fani mbalimbali.

"Tumeendelea na tutaendelea kukidhi mahitaji ya elimu kwa Vijana wetu wanaokuja kujiunga na Chuo chetu, na elimu ,ujuzi na stadi tunazowapatia wanafunzi wetu ni  pamoja na kuwaandaa wanafunzi wnaohitimu hapa chuoni  kupambana na soko la ajira na hata kuweza kujiajiri wengine"Amesema Boi.

Boi,amesema  kuwa mazingira ya ujifunzaji kwa chuo hicho  ni rafiki na wamekuwa wakipokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya Mikoa mengine.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.