DIWANI NDWATA AFANYA MKUTANO WA HADHARA WA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI WAKE
DIWANI wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Mhe. Eng. Hmais Ndwata, amefanya ziara ya kusikiliza kero, changamoto na maoni kutoka kwa wananchi wa Kata hiyo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Kihonda Maghorofani Sokoni Oktoba 08/2023.
Kupitia mkutano huo,Eng. Ndwata, ameweza kupokea kero na changamoto mbalimbali za wananchi zikiwemo kero za miundombinu ya barabara , huduma za kijamii huku baadhi ya kero akizipatia majibu na nyengibe kuzichukua kwa ajili ya utekelezaji.
Mikutano hiyo ya kusikiliza kero ni moja ya njia anayoitumia Mhe. Ndwata, kukutana na wananchi wake wa Kata ya Kihonda Maghorofani kutoka mitaa mbalimbali katika kushughulikia matatizo waliyonayo ikiwa pia ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya kuwataka Viongozi kushuka chini kusikiliza kero za wananchi wao.
Akijibu kuhusu kero ya Barabara, Eng. Ndwata, amesema Manispaa ya Morogoro bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 imetenge fedha kwa ajili ya kununua greda ambalo litasaidia kuboresha miundmbinu ya barabara.
Kuhusu upande wa huduma za afya, Eng. Ndwata, amesema huduma zote katika Zahanati ya Kata zinatolewa bure.
" Mtendaji nakuagiza nenda katengeneze kibao pale Zahanati kinachosema huduma za afya ni bure na weka namba yangu ili wananchi watakaosumbuliwa wanipigie simu yangu" Amesema Eng. Ndwata.
Aidha, amewashukuru watumishi wote wa Sekta mbalimbali wa Kata yake kwa kazi kubwa wanazozifanya za kuwahudumia wananchi.
Pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi CCM kwa usimamizi mzuri wa Ilani ya CCM kwani wamekuwa na msaada mkubwa wa kusimamia maendeleo ya Kata hiyo na kutoa maelekezo pale Serikali inapoteleza.
Mwisho, Eng. Ndwata, amewataka Watendaji wa Mitaa na Kata kushuka kwa wananchi kusikiliza kero zao badala ya wananchi kuja Ofisini au kuleta mabango ya changamoto zao wanapokuja Viongozi wa Serikali na Chama.
Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya na Kata, Wataalamu wa kutoka Ofisi ya TAKUKURU, NIDA pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa na viongozi mbalimbali wa vyuo vinavyozunguka Kata hiyo.
Post a Comment