Header Ads

DIWANI BUTABILE AWATAKA MADEREVA BODABODA NA BAJAJI KUFICHUA WAHALIFU


DIWANI wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, amewataka  madereva wanaoendesha Pikipiki (Bodaboda) na Bajaji kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kwenye vijiwe vyao. 


Kauli hiyo ameitoa Oktoba 6/2023 kwenye ukumbi wa Rose Garden kwenye kikao cha Viongozi waendesha Bajaji wa Kata hiyo.

Mhe. Butabile, amewataka waendesha Pikipiki (Bodaboda) hao kupiga simu wakati wowote Kituo cha Polisi au kumpigia yeye kwa kuwataja  watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

"Simu yangu ipo tayari kupokea taarifa zozote mlizo nazo zinazohusu vitendo vya kihalifu na nitazifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwalinda wale watakaonipa taraifa kwani Jeshi letu la Polisi lipo tayari kutoa usharikiano ili kuhakikisha Kata yetu inaendelea kuwa Salama" Amesema Mhe. Butabile.


Aidha,Butabile, amewataka  Bodaboda hao kutoa taarifa za madereva wa mabasi, malori na magari madogo wanaokiuka kwa makusudi Sheria za usalama barabarani ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na kupunguza matukio ya ajali za barabarani.

"Ajali nyingi husababishwa na madereva kutokuheshimu Sheria za barabarani, niombe tuzingatie sheria za barabarani pamoja na kuwa na nidhamu na uadilifu kwa lengo la kujijengea uaminifu kwa wateja hususani mavazi mnayovaa na kauli mnazozitumia kwa wateja wenu " Ameongeza Mhe. Butabile.

Mwisho, Mhe. Butabile , amewapongeza Waendesha Bajaji wa Kata ya Mafiga kwa kuunda Kikundi chao iliwa ni ishara nzuri ya kujiletea maendeleo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.