Header Ads

UWT Mkoa wa Morogoro yaadhimisha Wiki ya UWT na kuwataka wazazi kutoa malezi bora kwa watoto wenye mahitaji maalumu


WAZAZI  na walezi Mkoa wa Morogoro , wametakiwa kushirikiana na Vituo pamoja na Makao ya Kulelea watoto wenye mahitaji ili kuweza kusaidia huduma za Jamii.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania CCM Mkoa wa Morogoro  , Ndug. Alice Lubenanga, wakati  wa maadhimisho ya wiki ya UWT  walipo tembelea kwenye vituo na maeneo tofauti tofauti na a kutoa misaada ya mahitaji mbalimbali .

Aidha, Lubenanga, ameendelea kutoa wito kwa wazazi kujenga mazingila rafiki na watoto, pindi watakapowaona katika mazingira ambayo si ya makao au vituo ambavyo wanalelewa waweze kuwalejesha katika maeneo yao au kutoa taarifa kwa Walezi wa Viongozi wa maeneo yao.

Kwa upande wake, Katibu wa UWT Mkoa wa Morogoro, Ndug. Mwajabu Maguluko, amewashukuru akinamama wa UWT kwa kutenga muda wao na kuona umuhimu wa kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wenye mahitaji maalu







































No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.