Header Ads

ABOOD AKABIDHI MILIONI 1 KIKUNDI CHA MORO SUPER WOMEN KUENDELEZA MFUKO WAO.

MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Dkt. Abdulaaziz Abood, ametoa msaada wa fedha kiasi cha Sh. 1,000,000/= kwa Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali Mkoa wa Morogoro (MORO SUPER WOMEN ) ili  waweze kuongeza mtaji wa kuweza kusaidiana katika kujkwamua kiuchumi.

Akizungumza wakati akitoa msaada huo kwenye tukio la Kongamano la wakina mama hao lililojulikana kwa Women Supporting Women 2023 lililofanyika Ukumbi wa DDC Mbaraka Mwishehe Manispaa ya Morogoro Oktoba 22/2023, Mhe. Abood, amesema kuwa  anatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwasaidia wanawake hao ambao wanafanya shughuli za ujasiriamali.

"Nafanya jambo ili kwanza kutimiza matakwa ya Ilani ya Chama Chetu Cha CCM, lakini nimekuwa nikiguswa sana na Wajasiriamali ambapo mimi nikiwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini lengo ni kuona wakina mama Wajasiriamali wanapiga hatua na kufikia malengo yao " Amesema Mhe. Abood.

Mhe. Abood,  amekuwa akifanya hivyo kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wajasiriamali Mansipaa ya Morogoro licha ya baadhi ya vikundi ambavyo vimekuwa vikipewa mikopo kutoka Halmashauri yeye kama Mbunge wao ameona ni vema kuwaunga mkono kwa fedha kidogo ambazo Mungu amekuwa amembariki.

Pia, Mhe. Abood, ametoa muda wa matangazo wa kipindi cha wiki moja bure kwenye Kituo chake cha Habari cha Abood kwa wajasiriamali wanawake ili waweze kujitengenezea soko na kuongeza kipato.

Mwisho, Mhe. Abood, amesema  anaimani fedha hizo watazizalisha na kuweza kuwasaidia katika matumizi ya familia zao na pia kujiendeleza kwenye suala zima la maisha yao.

"Fedha hizi sijazikopesha ili warudishe , mimi ni Mbunge wa Vitendo,nimetoa fedha hizi  kama mtaji na ukikua wataendelea kukopesha katika vikundi vyao na mtaji utabaki kwenye kikundi" Ameongeza Mhe. Abood.

Akipokea msaada huo Mwenyekiti wa Moro Super Women, Neema Lusima, amesema fedha  hizo zimetolewa na mbunge huyo kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake wa Kikundi cha Moro Super Women , hivyo amempongeza na kumshiukuru kwa upendo wake na kuwajali wanawake wa Morogoro katika kukuza uchumi wao.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.