Header Ads

MH. ABOOD KUTOA DOLA 300 KUMSAIDIA MLEMAVU KUSHIRIKI TENIS UTURUKI.







MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, ameahidi kumasidia kijana Rehema Said kiasi cha Dola 300 sawa na shilingi laki 7 za kitanzania, ambaye anatarajia kuiwakilisha nchi katika mashindano ya wazi ya Tenis yatakayofanyika mji  wa Antalya Uturuki mwisho mwa mwaka huu Novemba 13-Desemba 02, 2022.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa yake, Mhe. Abood, amesema atahakikisha anafikisha salamu hizo kwa Viongozi wa nchi ikiwamo Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Rehema ni kijana pekee kwa ukanda wa Afrika Mashariki aiyechaguliwa kushiriki katika michuoano hiyo ya wazi ya Tenis.

"Najivunia kuwa na mshiriki anaeiwakilisha Afrika Mashariki kutokea katika Jimbo langu la Morogoro Mjini, ni bahati kubwa na salamu zake nitazifikisha kwa Viongozi wetu wa Kitaifa ikiwamo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuona namna ya kumsaidia kijana wetu kusafiri na kutimiza ndoto zake" Amesema Mhe. Abood.

Kwa upande wa Rehema, amemshukuru Mbunge Abood kwa jitihada zake za kumchangia fedha hizo ambazo zitasaidia kufanikisha safari yake ya kwenda kushiriki katika michuano hiyo nchini Uturuki.

Mwisho, Rehema, aliwahimiza na kuwaomba watu binafsi , viongozi mbalimbali na makampuni kujitokeza kumfadhili ili kufanikisha safari yake huku akiahidi kufanya vizuri katika mashindano hayo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.