Header Ads

DIWANI TUNDA AWATAKIA MITIHANI MEMA WANAFUZI DARASA LA SABA MWERE 'A' NA 'B'.









DIWANI wa Kata ya Kingo Manispaa ya Morogoro , Mhe. Amini Tunda, ametuma salamu za kuwatakia mitihani mwema wanafunzi wa darasa la saba  wa shule ya Msingi Mwere A na B na wanafunzi wa Manispaa ya Morogoro wanaofanya mitihani wa kumaliza elimu ya Msingi Oktoba 5-6/2022.

Salamu hizo zimetolewa na Mtendaji wa Kata ya Kingo, Maria Shine ,akimwakilisha Diwani wakati wa kuwatembelea wanafunzi hao na kugawa peni kwa wanafunzi wa shule zote mbili ambazo zimepata baraka kupitia dua mbalimbali.

Akiwasilisha salamu za Diwani, Maria, amesema Mhe. Tunda   anawatakia Kheri, Afya na Ufaulu katika mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi wanafunzi wote wa darasa la saba katika shule zote za Manispaa ya Morogoro hususani shule za Msingi Mwere A na B.

Mhe. Tunda amesema amewataka  wanafunzi kufanya mitihani hiyo kwa utulivu wa akili kuweza kufanya vyema na kuiletea sifa Kata ya Kingo na Manispaa kwa ujumla.

 “Nawatakia Mtihani mwema Wanafunzi wote wa wanaoanza Mitihani yao Oktoba 5-6/2022,   MUNGU wetu aliyemwaminifu awasaidie na awashindie katika mitihani yenu ,Mungu akawafanye Vichwa na Sio Mikia, Mungu awakumbushe kuandika majibu sahihi, Mungu akatoweshe magonjwa na roho za uoga wakati huu wa mitihani.”Amesema Mhe. Tunda.

Mhe. Tunda,amesema , kuwa ana amini walimu wamefanya kazi yao kwa kipindi cha miaka saba shuleni kwa wanafunzi hao na sasa ni wakati wa wanafunzi kuhakisha kwamba waliyojifunza kwenda kuyafanyia kazi katika mitihani hiyo ili waweze kufaulu vizuri na kuiletea sifa wilaya ya Kilolo na wazazi wao kwani elimu ya msingi ndio mwanzo wa maisha mazuri endapo watafanya vyema.

Aidha, Mhe. Tunda, amesema endapo mwanafunzi akitulia katika kufanya mitihani hiyo kuna uhakika mkubwa wa kufanya vyema na kufaulu kwani mitihani hiyo inatolewa katika masomo ambayo wamefundishwa kipindi chote wakiwa shuleni ni suala la kujiamini na utulivu wa akili na kama mmejiandaa Vizuri mtapata Matokeo Chanya.

Katika salamu hizo, Afisa Mtendaji aliambatana na Afisa Elimu Kata ya Kingo Bi. Happiness Odoyo, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Kingo, Sezaria Mrema huku wakichangia kiasi cha shilingi 40000 kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi hao.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.