Header Ads

DR. SIMBA AITAKA JUMUIYA YA WAZAZI CCM KUSHIKAMANA KULINDA DOLA .

JUMUIYA  ya Wazazi Tanzania chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini  imetakiwa kushikamana kuwa wamoja katika kutetea chama chao ili kiendelee kushika dola .

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa, Dr. Ally Simba , katika Mkutano wa ufunguzi wa Baraza la Wazazi la kumchagua Katibu wa Elimu ,Malezi na Mazingira lililofanyika Oktoba 18/2022,  Ukumbi wa  Glonecy Hotel Nanenane Kata ya Tungi.

“Nawaomba wana Jumuiya ya Wazazi wote wa CCM Mkoa wa Morogoro hususani Wilaya ya  Morogoro Mjini, tunatakiwa kushikamana kujenga chama na Jumuiya yetu kwa dhumuni la kushirikiana kuakikisha chama kina shika dola ”Amesema Dr. Simba.

Kwa upande wa Katibu wa Wazazi Mkoa wa Morogoro, Ndg. Zuberi Mtelela,  amesema jukumu la kwanza la Jumuiya ya Wazazi ni kuhakikisha kinatetea chama kiweze kushika dola na kuibuka na ushindi mnono katika chaguzi mbalimbali.

Mtelela,amewataka wanajumuiya kufanya kazi badala ya kuendekeza majungu yanayolenga kuipasua jumuiya na kushindwa kufikia malengo.

Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Amiri Mkalipa,  amewataka wana CCM kuondoa makundi ndani ya chama kwani si wakati wake kwa sasa badala yake amewataka wana CCM kujenga chama .

Naye Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Morogoro Mjini, Salum Kipira,amesema Jumuiya imekuja kivyengine hivyo kila mtu atimize wajibu wake huku akiwataka wana CCM wa jumuiya hiyo waache tabia ya kupanga safu ya wagombea kwani kampeni bado hazijaruhusiwa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.