ABOOD AKABIDHI KITANDA CHA WAGONJWA WA UPASUAJI
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, amekabidhi Kituo cha Afya cha Sabasaba Kitanda cha wagonjwa wa upasuaji pamoja na taa zake ikiwa ni moja ya kuboresha Sekta ya afya.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi kitanda hicho , Mhe. Abood, amesema lengo la kutoa kifaa hicho ni kuendela kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu hassan za kuboresha huduma za afya nchini.
Mhe. Abood, amesema amekua akiumizwa sana na changamoto zinazowakabili wananchi ambazo amekua akikutana nazo kila anapokuwa katika ziara zake za kikazi kuwatembelea wananchi hasa changamoto zilizopo katika sekta ya afya zikiwemo mazingira bora ya kujifungulia kina mama na vitanda vya kulalia wagonjwa.
" Nimekuwa nikifanya ziara za kikazi katika Jimbo langu,za kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa msaada wa serikali na wakati mwingine kwa kutumia fedha zangu, leo nipo hapa kukabidhi Kitanda hiki ambacho Rais Samia amenituma nilete ikiwa ni mkakati wa kuoboresha huduma za afya , nampongeza sana Rais wetu kwa kuwa mstari wa mbele hususani katika upande wa afya ikiwamo kuboresha huduma ya mama na mtoto" Amesema Mhe.Abood.
Mwisho, Mhe. Abood, amesema kuwa ataendela kushughulika na changamoto za huduma za afya kwani amepanga kila Kituo cha afya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa ambapo kwa sasa Kituo cha afya cha sabasaba kilishapatiwa gari lake la kubebea wagonjwa ( Ambulance).
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr. Charles Mkumbachepa, amemshukuru Mbunge Abood kwa jitihada zake za kuboresha huduma za afya huku akimuahidi Manispaa kuendelea kumuunga mkono na kutoa ushirikiano.
Post a Comment