Header Ads

KAMATI NDOGO YA AFYA MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA AFYA .


KAMATI ndogo ya  afya Manispaa ya Morogoro ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Aisha Kitime,  imefanya ziara ya kukagua miradi ya afya inayotekelezwa katika Manispaa hiyo na kutoa pongezi za uendeshaji wa miradi kwa kuzingatia viwango ikiwemo  ubora wa majengo pamoja na kasi ya uendeshaji.

Kauli hiyo imetolewa Oktoba 06/2022 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Aisha Kitime wakati wa ziara ya kukagua miradi ya afya ikiwamo Zahanati na Vituo vya afya katika kuona huduma zinazozotolewa kwa wananchi.

Mhe. Kitime,amesisitiza muda uliopangwa wa uendeshaji wa miradi kukamilika uendelee kuzingatiwa na katika maeneo ambayo yameonekana kuna changamoto yafanyiwe kazi pamoja na kuboresha  huduma za afya katika vituo hivyo.

"Tumetembelea miradi yetu ya afya, lengo la kamati hii ndogo  ni kusaidia kamati kuu ya afya kufanya kazi kwa urahisi,  ,tumeona ubora wa majengo ni mazuri na wauguzi wetu wanajitahidi kuwahudumia wagonjwa, kikubwa niombe kuwasisitiza  waganga wafawidhi katika Vituo kuwashirikisha viongozi wenu wa ngazi ya kata  kwenye Kila hatua kuepusha kutokea kwa changamoto mwishoni" Amesema Mhe. Kitime.

Mhe. Kitime, amewataka Waganga wafawidhi kuhakikisha katika vituo vyao kuna  vifaa tiba vidogovidogo huku wakiendelea kusubiria vifaa vyengine vya huduma.

Mwisho wajumbe waliendelea kusisitiza katika changamoto zilizopatikana kwenye baadhi ya miradi kutiliwa mkazo kuhakikisha zinafanyiwa kazi ikiwa ni moja ya kazi ya kutimiza majukumu ya kamati.

Miradi iliyotembelewa na kamati ndogo ya afya ni pamoja na Kituo cha afya cha Tungi, Zahanati ya Magaza Mindu, Zahanati ya Kihonda Maghorofani, Zahanati ya Uwanja wa Taifa, Zahanati ya Kiwanja cha Ndege, Sultan Area pamoja na Zahanati ya Mbuyuni.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.