DKT. MOLLEL AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUHAMASISHA LISHE BORA KWA JAMII.
NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewataka viongozi wa dini nchini kutoa Elimu ya lishe bora kwa waumini wao kwa lengo la kuhamasisha matumizi bora ya chakula na kuwa na afya bora ili kuleta maendeleo yao na taifa kiuchumi na kijamii.
Waziri Mollel amesema hayo Oktoba 29, mwaka huu wakati wa Maaadhimisho ya siku ya lishe kitaifa yaliyofanyika Mkoani Morogoro katika uwanja wa Mpira wa Fulwe Tarafa ya Mikese Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Akitoa hotuba mbele ya mamia ya watu walioshiriki maadhimisho hayo Dkt. Mollel amesema kama nchi inataka kuwa na taifa la wasiopenda dhambi na kama linataka kuwa na taifa la wacha mungu ni lazima kushughulika na uwezo wa akili za watu huku akiwaomba viongozi wa Dini kuongelea suala la lishe wakati wa ibada zao.
“… Maadhimisho ya lishe kitaifa yanafanyika Mkoani Morogoro, nikili tu kwamba Morogoro ni miongoni mwa Mikoa kumi ambayo haijafanya vizuri katika suala zima la lishe..” amesema Fatma Mwassa.
Akibainisha hayo amesema udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano katika mkoa huo umefikia asilimia 26.4, upungufu wa damu kwa watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 ni asilimia 29.8 hivyo Mkoa upo miongoni mwa mikoa ambayo inatakiwa kusaidiwa katika kuboresha lishe ndani ya jamii.
Akibainisha hayo amesema udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano katika mkoa huo umefikia asilimia 26.4, upungufu wa damu kwa watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 ni asilimia 29.8 hivyo Mkoa upo miongoni mwa mikoa ambayo inatakiwa kusaidiwa katika kuboresha lishe ndani ya jamii.
Ili kukabiliana na udumavu huo na utapiamlo amemhakikishia Mgeni rasmi kuwa tayari amesaini mkataba wa lishe na wakuu wa Wilaya, na Wakuu wa Wilaya nao wamesaini mkataba huo na Wakulugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo kwa lengo la kuboresha lishe.
Mwanamasumbwi maarufu kama Mandonga alikuwepo kuhamasisha kuhamasisha wananchi kula chakula chenye mchanganyiko kamili ili kuwa timamu zaidi kiakili na kimwili, huku akidai ngumi zake aina ya Ndoige zinatokana na Lishe Bora anayopata kwa kila siku. hapa anasalimiana na mgeni rasmi baada ya kusema neno kwa wananchi.
Akizungumzia juu ya jitihada za Serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha sekta ya Afya, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa Mkoa umepokea kiasi cha shilingi Bilioni 22 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika Mkoa huo, huku hospitali ya Rufaa ya Mkoa imepokea zaidi ya shilingi Bilioni tatu kwa ajili ya kuboresha hospitali hiyo huku akibainisha kuwa mipango ya baadae ni kujenga jengo la ghorofa ambalo litatoa huduma zote.Mwisho ameendelea kutoa wito kwa wananchi kujiunga na bima ya afya kwa lengo la kupunguza gharama za matibabu.
Katika hatua nyingine Fatma Mwassa amewataka wadau wa lishe kujikita katika kutoa elimu ya lishe mashuleni kwa kutumia ujumbe mbalimbali kupitia tv “online’ kwa kufanya hivyo elimu ya lishe itawafikia wengi.
Post a Comment