ABOOD AUNGA MKONO KIKUNDI CHA UARIDI KWA KUCHANGIA MILIONI 1.
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, amechangia kiasi cha shilingi Milioni 1 kwa Kikundi cha Uaridi kilichopo Kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro .
Mchango huo ameutoa Oktoba 06/2022 akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kikundi hicho ambapo Mhe. Abood ametoa fedha hiyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada walizozionyesha katika kupambana au kujikwamua kiuchumi ili kutunisha kidogo mfuko wao.
Aidha, Mhe. Abood, amesema faida ingine kubwa ya kuwa kwenye kikundi ni kwamba itakuwa rahisi kuwashawishi wataalamu wa fani mbalimbali kuja kutoa huduma za mafunzo kwa kikundi cha watu wengi kuliko kwa mtu mmoja.
Mwisho, Mhe. Abood, amevitaka vikundi vya uzalishaji kuzalishaji bidhaa kwa gharama nafuu pamoja na kujiepusha na migogoro ikiwamo kuwa na viongozi imara.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Kichangani, Mhe. Gilbert Mtafani, amekitaka Kikundi cha Uaridi, kuwa na matirio yenye ubora ili kuleta ushindani katika masoko.
Naye Mkurugenzi wa TAPEC, Leons Mvungu, amemshukuru Mbunge Abood huku akiahidi kuvisimamia vikundi vyote kwa kufuata misingi ya sheria ili vifikie malengo yao.
Mvungu, amesema licha ya kuwepo kwa vikundi vingi vidogo vya fedha, lakini bado kuna changamoto kama vile ukosefu wa eneo la kutekeleza miradi , mitaji ya kuendesha shughuli za miradi yao pamoja na masoko.
Post a Comment